1
 Meneja wa Fhi Tulonge Afya Kanda Kaskazini na Kati, Dkt. Benedict Kafumu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo ya awali ya namna ya utoaji taarifa kwa jamii juu ya majukwaa mawili yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya NAWEZA NA ITETELEKI. Mafunzo hayo yamefanyika leo katika Hoteli ya Ristalemi mjini Tabora.
2
 Afisa wa Afya kutoka Wizara ya Afya, Oscar Kapera akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ​mafunzo ya awali ya namna ya utoaji taarifa kwa jamii juu ya majukwaa mawili yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya NAWEZA NA SITETELEKI.Mafunzo hayo yalifanyika leo katika Hoteli ya Ristalemi mjini Tabora.
3
Mtaalamu Mkongwe wa Ushauri wa mambo ya Afya kutoka Fhi Tulonge Afya, John Bosco Basso akizungumza jambo wakati wa ​mafunzo ya awali ya namna ya utoaji taarifa kwa jamii juu ya majukwaa mawili yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya NAWEZA NA SITETELEKI.  

WIZARA ya Afya kwa kushirikiana na Mradi wa USAID Tulonge Afya fhi 360 wametoa mafunzo kwa wanahabari mkoani Tabora juu ya utoaji habari baada ya uzinduzi wa majukwaa mawili ya mawasiliano ya afya kwa watu wazima ‘NAWEZA’ na vijana ‘SITETELEKI’ yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

Majukwaa hayo yanalenga kufikisha elimu sahihi itakayoijengea jamii ya Watanzania uwezo ili kubadilisha mitizamo na tabia zao za kiafya na kuleta matokeo chanya.

Mafunzo hayo yamendeshwa na wataalamu wa masuala ya afya kutoka Wizara ya Afya na USAID Tulonge Afya fhi 360 yalifanyika leo katika Hotel ya Rastalemi mjini Tabora na kupata mwitikio mkubwa na uelewa mzuri kwa wanahabari wa mkoani humu yakiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa majukwaa hayo ya NAWEZA na SITETEREKI mkoani humo.

Mtaalamu wa mambo ya Afya kutoka Wizara ya Afya, Oscar Kapera alisema NAWEZA ni jukwaa linalolenga kuwafikia wananchi tofauti tofauti na itachangia kuboresha afya na ustawi wa Watanzania wengi, itakuwa ikibadilika badilika ili kukidhi mahitaji ya maeneo mengine ya kiafya muhimu kwa walengwa hao ama makundi mengine hususani watu wazima. Toggle screen reader support
Share To:

msumbanews

Post A Comment: