Afisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Esther Luvanda akitoa maelezo kuhusiana mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na namna ya kuresha mkopo walipokwenda kutoa elimu ya masuala ya mikopo kwa wanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari Benjamini Mkapa.
Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Daud Elishaakizungumza na wanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari Benjamini Mkapa walipokwenda kutoa elimu ya masuala ya mikopo.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa wakiwasikiliza maafisa wa Bodi.
Mwanafunzi wa Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa Charles Mwamwenda akizungumza na waandishi habari namna walivyopokea ujio wa bodi.
Na Chalila Kibuda,
Wanafunzi wameaswa kuwa makini katika ujazaji wa maombi ya mkopo wa elimu ya juu katika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Akizungumza na wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari Benjamini Mkapa Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Daud Elisha amesema bodi iko kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa wale wanaohitaji.
Daud amesema kuwa wale ambao wataomba baada ya kuchaguliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) wanapeleka majina bodi ambao ndio wanaanza kuchakata mikopo kwa wahitaji wa mikopo hiyo.
Aidha amesema kuwa waombaji wote lazima wazingatie vigezo vilivyoanishwa kwani bodi haina uwezo kutoa mkopo kutokana na kukosekana kwa taarifa za huo mkopo. Nae Afisa Bodi hiyo Esther Luvanda amesema mkopo wa kutoka bodi lazima ulipwe ili kuweza kusomesha wengine.
Amesema kuwa wanafunzi wahakikishe wanaambatanisha taarifa zinzohitajika zilizo sahihi.
Mwanafunzi wa Kidato cha Sita shule ya Sekondari Benjamini Charles Mwamwenda amesema bodi wamefika wakati mwafaka kwani wanajuaga changamoto ya wanafunzi waliopita hivyo elimu hiyo itawasaidia kufanya vizuri.
Post A Comment: