Na. Ferdinand Shayo,Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fabian Gabriel Daqqaro amefunga rasmi mafunzo ya jeshi la akiba lililoshirikisha zaidi ya wanafunzi 300 huku akiwataka jamii kuacha fikra potofu kuwa wanaosomea mafunzo ya ugambo wanapoteza muda badala yake wawape nafasi zaidi vijana katika kusomea mafunzo hayo kwani yana fursa nyingi za ajira.
Hayo yamesemwa wakati wa kufunga mafunzo ya jeshi la akiba lililofanyika katika viwanja vya gymcana mkoani arusha ambapo mkuu wa wilaya ya arusha fabian daqqaro amekemea vikali tabia ya upotofu unayofanywa na baadhi ya watu nchini kuwa jeshi hilo la akiba halina msaada wowote nchini na kuwaoondoa hofu wanafunzi hao kuwa mafunzo waliyo yapata yanafursa nyingi za ajira kwani hawezi kupataajira bila kupitia mafunzo ya jeshi la akiba.
Aidha mheshimiwa Daqqaro wamewataka wanafunzi waliohitimu mafunzo ya hayo kuzingatia nidhamu na kutumia mafunzo walioyapata katika kulinda jamii na mali zao,pamoja na kupinga rushwa, nakujihusisha katika makundi hatarishii huku akiwataka makampuni na viongozi mbali mbali kuwapa nafasi za ajira vijana hao waliohimu kwani wanaweredi katika kulinda na kupambana na uharifu.
"Kuna jambo linaudhi sana ambalo nalisikia sana kwa watu mara nyingi wanasema wagambo hawana msaada wowote lakini mimi niwaambie jambo wagambo wana umuhimu mkubwa katika taifa la Tanzania,na sasa tunaweka utaratibu na ofisi ya mkoa kwa wale ambao wameajiriwa katika maofisi na makampuni na hawajapitia jeshi la akiba hao hawatakuwa na sifa ya kupata ajira mpaka ujiunge na jeshi la akiba’ alisema
Sambamba na hayo Mkuu wa Wilaya ya Arusha Daqqro amewapatia ajila wanafunzi Zaidi ya 200 waliomaliza mafunzo kupitia ahadi ya makampuni ya ulinzi waliojitokeza katika sherehe hiyo yakufunga mafunzo hayo
Aidha baadhi ya wanafunzi waliomaliza mafunzo hayo wamesema kuwa wamefurahishwa sana maneno mazuri ya kutia moyo kutoka kwa mkuu wa wilaya arusha kwani jeshi la akiba watu hawalithamini na kuliona kama halifai lakini maneno hayo yamewatia faraja .
Post A Comment: