Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akitoa pole kwa wazazi waliofiwa
na watoto wao alipotembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa mara tu
baada ya kupata taarifa ya vifo vya watoto wawili na mmoja kuwa mahututi
baada ya kupatikana tangu kupotea kwao tarehe 21.3.2019.
Eneo la Nyumba ya mtuhumiwa ambaye ni Mganga wa Kienyeji wa mtaa wa Vuta, Kata ya Kizwite mjini Sumbawanga baada ya nyumba hiyo kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kubaini kuwa mganga huyo amesababisha vifo vya watoto wawili na mmoja kuwa mahututi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Vuta Sangu Sokoni juu ya tukio la kupotea kwa watoto watatu na hatimae kupatikana wawili wakiwa wamefariki na mmoja kuwa mahututi akiendelea na matibabu.
-Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akionyesha eneo katika nyumba iliyokuwa haijamalizika ambapo maiti za watoto hao zilipatikana baada ya kutupwa na mtuhumiwa James Kapyela ambae ni mganga wa kienyeji.
Diwani wa Kata ya Kizwite ambae pia ni mchungaji Felician Mavazi (alipiga magoti) akiomba muda mfupi kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo kuongea na wananchi wa mtaa huo wa Vuta kata ya Kizwite juu ya tukio la mauaji ya watoto wawili.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alipokuwa akiongea na wananchi wa mtaa wa Vuta, Kata ya Kizwite Sumbawanga mjini. |
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo amemuagiza
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa ACP Mathias Nyangi kuhakikisha anafanya msako
wa waganga wa kienyeji katika mkoa na kuwakamata wale wote wanaofanya uganga wa
kienyeji bila ya kuwa na leseni halali za kuwaruhusu kufanya shughuli hizo.
Ametoa agizo hilo baada ya kusikiliza vilio vya wananchi wakati
wa mkutano ulifanyika mtaa wa Vuta, Kata ya Kizwite, mjini Sumbawanga, wananchi
waliokuwa wakiomboleza vifo vya watoto wawili na mmoja kubaki mahututi katika
hospitali ya rufaa ya mkoa baada ya mganga wa kienyeji kuwateka na kuwaficha
katika gari lake chakavu tangu watoto hao kupotea tarehe 21.3.2019 na wawili kupatikana
wakiwa wamefariki tarehe 23.3.2019 baada ya mmoja aliyepona kutoroka na
kuwajulisha wananchi kilichotokea.
Amesema kuwa msako huo wa waganga wa kienyeji ufanyike
katika wilaya zote tatu za mkoa ili kuwahakikishia wananchi amani na utulivu
ambayo imekuwepo kwa miaka yote na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano katika
kuhakikisha wanawafagia waganga hao wanaonyesha dalili za kuvuruga utulivu
uliopo katika mkoa.
“RPC fanya Operesheni kali ya waganga wa Kienyeji ndani
ya Mkoa huu, wale ambao wana leseni tutajua hukohuko kwamba huyu ana leseni n
ani halai au siyo halali na kama sio halali basi huyo ni halali yako, na kama
kuna mganga wa kienyeji asiye na leseni, huyo ndio kabisa halali yako zaidi,
kuanzia sasa hivi bonde la ziwa Rukwa kule Nkasi, Kalambo, Sumbawanga yenyewe
hapa kote, opresheni ipite ya kamatakamata waganga wa kienyeji, tumechoka,”
Alisisitiza.
Wakati wakitoa malalamiko yao kwa mkuu huyo wa mkoa,
wananchi hao walisema kuwa vifo vya watoto hao vinahusishwa na Imani za
kishirikina ambapo kumekuwa na wimbi la vijana wanaoonekana wakila, wakinywa na
kuvaa vizuri bila ya kujulikana shughuli zao maalum wanazofanya jambo mbalo
limekuwa likiwaumiza kichwa wananchi hao na kukosa majibu.
Mmoja wa wananchi hao Debora Maenge alisema “ Nasikitika
kwa tukio hili lililotokea mtaa wa Vuta, huyu mtu tunaishi nae jirani sana,
tunajua ni mtu mwema, kumbe ni mtu ambae sio mwema na hafai kabisa katika
jamii, cha kushanga alikuwa na vibali ambavyo alikuwa akijitambulisha kuwa yeye
ni mganga wa jadi, vibali hivi vinatolewa serikalini, Je serikali yetu
mtaendelea kutoa vibali hivi ili watu waendelee kuuawa kiasi hiki? serikali
angalieni mnapotoa vibali je ni waganga Kweli?” Aliuliza.
Mh. Wangabo alitembelea eneo la nyumba ya mganga huyo wa
kienyeji ambayo gari alilowafichia watoto ilikuwamo na kukuta nyumba hiyo ikiwa
imevunjwa na gari la mganga huyo kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali.
Watuhumiwa James Kapyela (52) pamoja na mtoto wake Michael
Martin (14) wa tukio hilo la mauaji ya watoto Nicolous Mwambage (7) pamoja na
Emanuel Juma (4) hivi sasa wanashikiliwa na polisi huku uchunguzi wa awali
ukionyesha watoto hao walifariki kwa kukosa hewa baada ya kufungiwa ndani ya
gari chakavu aina ya Chaser Saloon iliyokuwa haitumiki na vioo vya gari hiyo
kufungwa.
Post A Comment: