Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi ya Kilimo Bwana Paulo Tarimo wakati akiwasilisha mada kwenye ukumbi wa mkutano wa Misitu uliopo Kihonda Morogoro jana 11.03.2019 

Wataalamu kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali wamekutana katika Ukimbi wa Misitu uliopo Kihonda Mkoani Morogoro lengo likiwa ni kujadili Sheria ya kusimamia eneo litakalotengwa kwa ajili ya shughuli za  Kilimo ambayo inatarajiwa kuimarisha sekta hiyo kwa kuleta tija kubwa  kwa wakulima na kuongeza uwekezaji.

Akiongea katika Mkutano huo wa siku mbili mgeni Rasmi katika mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe amewashauri wataalamu hao kuhakikisha rasimu ya Sheria hiyo haingiliani na Sheria nyingine zinazosimamia ardhi.

Aidha migogoro mingi baina ya wakulima imekuwa ikisababishwa na ukosefu wa Sheria ya kulinda na kusimamia matumizi ya ardhi ya Kilimo hivyo kila Mtu kufanya anavyotaka alisistiza Mkuu wa mkoa.

Hata hivyo  katika kikao hicho ambacho kimetumika  kuchukua maoni ya wadau Dkt Kebwe amesema uwepo wa Sheria ya usimamizi wa ardhi ya Kilimo ni  muhimu katika usimamizi na  uendelezaji wa  sekta hiyo hasa kwa wakati huu nchi inapoingia katika uchumi wa Viwanda.

"Moja ya changamoto ninazozipata kwenye ofisi yangu ni kuitambua ardhi ya Kilimo, wanakuja wawekezaji  kwenye kilimo lakini kukosekana kwa sheria kama hii inayoonesha ardhi ya kilimo Kwa ajili ya matumizi ya  wananchi na wawekezaji inakuwa ni changamoto kubwa." alisema Mkuu Wa mkoa Dkt Kebwe Stephen .

Alisema mipango inayoendelea kutekelezwa na serikali kupitia wizara ya Kilimo inaonesha nchi inaweza kulisha mataifa mengine ya Afrika na nje ya bara hili ambapo Sera na Sheria zitatumika kuimarisha Kilimo na kuwalinda wakulima wetu alisisitiza Mheshimiwa mkuu Wa mkoa.

Naye Mkurungezi wa kinalindaMipango na Matumizi Bora ya Ardhi ya Kilimo Bw Paulo Tarimo amesema mchakato wa kuandaa Sheria ya Kilimo ni muhimu kwa kuwa utasaidia kuitambua ardhi ya Kilimo ki Sheria pamoja na Sheria.

Akiwasilisha mada yake Mkurugenzi huyo amesema hakuna kipengele ambacho kinalinda ardhi ya Kilimo hivyo Sheria hii ni muhimu kwa sababu pamoja na kusimamia matumizi bora ya ardhi lakini itasaidia mipango mbalimbali ya kalimo.

Gungu Mibavu Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipago akimwakilisha Mkurugenzi wa Idara hiyo amesema wazo La kuwa na Sheria ya usimamizi wa ardhiya  Kilimo lilianza toka 2009 ambapo michakato mbalimbali imeendelea ili kupata Sheria hiyo.

Aidha Sheria hiyo itasimamia shughuli zote za ugani ardhi ya Kilimo na taratibu zote za zana za kilimo

Awali Mkurugenzi Mtendaji kutoka Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania MVIWATA Bwana Stepen Ruvuga amesema kwamba sheria hii inatakiwa kuwa na maslahi mapana kwa wakulima kwa kuwa Kilimo pamoja na kwmba ni kichocheo cha maendeleo lakini pia ni uhai wa wakulima wadogo.

Hata hivyo Bwana Stephen Ruvuga amesema Sera nyingi pamoja na baadhi ya Sheria zimeandaliwa  pasipo kumshirikisha mkulima mdogo na kuangalia mahitaji yake lakini zimekuwa zikijali maslahi ya wakulima wakubwa na wawekezaji hivyo Sheria hii inaweza kuwa na tija  kwa sababu imekuwa shirikishi.

MWISHO
-- Mathias Canal Chief Executive Officer (C.E.O) WAZOHURU MEDIA GROUP LIMITED canalmathias@gmail.com wazohuru14@gmail.com 0756413465 www.wazohuru.com
Share To:

Post A Comment: