Wabunge wawili wa CHADEMA, Susan Kiwanga wa Mlimba, na Peter Lijualikali wa Kilombero wamerudishwa rumande na mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro ambapo wanasubiri hadi Marchi 7, 2019 itatoa uamuzi wa dhamana yao.
Kiwanga na Lijualikali walifikishwa Mahakamani hapo jana ambapo kesi yao ilianza kusikilizwa kupitia kwa Hakimu Elizabert Nyembele.

Utakumbuka hadi sasa Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko wako rumande kutokana na makosa ya kukiuka masharti ya dhamana.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: