Majukwaa ya Vijana yaliyoko katika kata mbalimbali za Wilaya ya Arusha yameshiriki katika maonyesho ya Ujasirimali yaliyoandaliwa na shirika lisilokua la kiserikali la Infoy ambapo vijana hao wameonyesha shughuli za ufugaji wa samaki na bidhaa za usindikaji.
Mratibu wa Shirika lisilokua la kiserikali la INFOY, Laurent Sabuni alisema kuwa Maonyesho hayo yanalenga kuhimiza ushiriki wa vijana katiika uchumi wa viwanda na kuongeza kuwa kutokana na vijana kuchangamkia fursa ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo suala la vifungashio linapaswa kutiliwa mkazo ili kuinua ari ya uzalishaji .
Sabuni alisema kuwa Majukwaa ya vijana ni moja ya njia muhimu ya kuwakusanya vijana na kuwaweka pamoja ili waweze kupata mafunzo ya ujasiriamali pamoja kuwafikia vijana wengi ambao wana nia ya kusonga mbele kiuchumi.
“Vijana wakiwa katika vikundi ni rahisi kusaidika tofauti na kuwafikia kijana mmoja mmoja inakua ngumu hivyo ni vyema vijana wakajiunga kwenye vikundi” Alieleza Sabuni
Mjasiriamali Goodness Shayo Alisema kuwa maonyesho hayo yatasaidia kuinua ari ya vijana kujikita katika shughuli za uzalishaji badala ya kuwa walalamikaji na pia kuondokana na kasumba ya kuchagua kazi.
Alisema kuwa mkoa wa Arusha vijana wamekua wakizalisha bidhaa mbali mbali licha ya uhaba wa viwanda vya kutengeneza vifungashio vya bidhaa suala linalowazimu kuagiza kutoka mikoa mingine hivyo kuongeza gharama za usafirishaji na kuathiri bei ya bidhaa zao katika soko.
Goodness ameiomba serikali na taasisi binafsi kuungana kutatua changamoto hiyo kwa kuanzisha viwanda vya kutengeza vifungashio kutokana na mwamko wa vijana wa kuchangamkia fursa za uchumi wa viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya usindakaji wa nafaka.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabiel Daqqaro akipata Maelezo juu ya bidhaa zinazozalishwa na vijana kutoka Majukwaa ya Vijana Wilaya ya Arusha yaliyoandaliwa na shirika lisilokua la kiserikali la INFOY.
Post A Comment: