Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga akizungumza wakati wa ziara hiyo |
Diwani wa Kata ya Mnyanjani (CUF) Thobias Haule akizungumza katika ziara hiyo |
Sehemu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali wakifuatilia mkutano huo wa Waziri Mpina na Wavuvi eneo la soko la Samaki la Kasera Jijini Tanga |
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina kushoto akisisitiza jambo kwa mmoja wa wavuvi waliopo eneo hilo mara baada ya kuzungumza nao |
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akiagana na wavuvi wa eneo la soko la Kasera Jijini Tanga mara baada ya kumaliuza kusikiliza kero zao zinazowakabili wakati wa ziara yake |
Mmoja wa wavuvi Jijini Tanga akiuliza swali kwa WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina
NA MWANDISHI WETU, TANGA.
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amesema serikali imefanikiwa kuutokomeza uvuvi haramu kwa kutumia mabomu kwa kiwango kikubwa cha zaidi ya asilimia 98 huku wakiendelea kupambana kuhakikisha unakwisha kabisa kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mpina aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani Tanga iliyokuwa na lengo la kukutana na wavuvi kwenye soko la Sahare Kasera Jijini Tanga na Moa wilayani Mkinga ikiwa ni kusikiliza kero zinazowakabili na kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi.
Ziara hiyo inatokana na wito wa viongozi waliotaka afike kwenye eneo hiloi ili kuweza kubaini changamoto zinazowakabili wavuvi hao na kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi wa kina.
Alisema baada ya kufanikiwa kuutokomeza uvuvi wa mabomu hivi sasa wanageukia kwenye nyavu haramu kwa kuhakikisha zinaondolewa majini ili wananchi waendelee kuvua kwa njia endelevu itakayokuwa na tija kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
“Niwaambie kwamba nyavu haramu zilizokamatwa kwenye ukanda wa bahari kuu ukizibadilisha ni zaidi ya km 773 zimekamatwa zilzokuwa zinavua kwa njia haramu…leo hii watu walipokuwa wanavua na sumu samaki wanateketea, watanzania wanapoteza maisha kutokana na uvuaji wa namna hii na tusipojipanga vizuri kuzilinda rasilimali za bahari zitatoweka “Alisema Waziri Mpina
Aidha alisema kutokana na uvuvi huo haramu leo hii zaidi ya bilioni 56 ya fedha za kitanzania wanazitumia kuagiza samaki kutoka nje wakati nchi ina maziwa mengi na bahari kubwa, mito mingi mikubwa ambayo ingeweza kutosheleza mahitaji.
“Haiwezekani kuagiza samaki kutoka nje hata kwenye nchi ambazo hazina mabwawa wala mito kutokana na sisi samaki wetu tunawavua kwa mabomu na sumu, makokoro hivyo kwa pamoja lazima tubadilike na tukubaliane kuzilinda rasilimali zetu”Alisema Waziri Mpina.
“Lakini pia niwaambie kwamba serikali ya awamu ya tano ipo pamoja na wananchi wake ndio maana leo hii waziri nimekuja hapa na watendaji wengine wa serikali kuwasikiliza mnachangamoto gani pamoja na hayo niwaambie mnapoona serikali inachukua hatua kwa ajili ya rasilimali hizo mjue ni kwa ajili yenu”Alisema.
Alisema serikali inapochukua hatua mbalimbali za kukabiliana na uvuvi haramu mtambue inafanya hivyo kwa ajili ya nia nje ya kuhakikisha rasimali zilizokuwepo majini zinalindwa ili kuepusha zisitoweke.
“Wapo wavuvi wanavua kwa nyavu halali na wapo wengine wanavua kwa nyavu haramu ukienda kuvua kwa mabomu na nyavu haramuni hatari kubwa kutokana na kuharibu mazalia ya samaki na viumbe vyengine vilivyopo majini lakini pia kuhatarisha afya za walaji kutokana na kwamba wanaweza kupata saratani”Alisema
Awali akizungumza katika ziara hiyo, Mkurugenzi Msaidizi Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi Mchira Wamarwa alisema katika operesheni ya biashara haramu ya samaki na mazao yake uliofanyika ukanda wa pwani ya bahari ya hindi kwa siku 29 kutokana na ukanda huo kuna matukio mengi
Alisema uendelevu wa rasilimali za uvuvi bahari ya hindi unatishiwa na uwepo wa uvuvi unaofanyika kinyume cha sheria ya uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni za mwaka 2009 pamoja na sheria nyengine za nchi ikiwemo wa sheria za mazingira namba 20 ya mwaka 2004.
Alisema uvuvi haramu unaofanyika kwenye bahari ya hindi ni matumzi ya zana haramu na mbinu haramu za uvuvi, matumizi ya milipuko,kuvua bila leseni ,matumizi ya nyavu zenye macho chini ya nchi tatu, vyavu za timber,njavu za dagaa zenye macho chini ya milimita 10,uvuvi wa katubi ,kutumia vyombo visivyoisajiliwa na kuvua kwenye maeneo yasiyosajiliwa
Awali akizungumza Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alisema katika Jiji hilo wanachokiwanda kiwanda kimoja kinachochakata samaki ambacho kinakabiliwa na changamoto ya kutokupata samaki wa kutosha wanakusanya kidogo kidogo hali inayopelekea kufanya kazi mara moja kwa wiki au wiki mbili ndio wanachakata.
Alisema kutokana na kuwepo kwa hali hiyo siku nyengine wanakusanya kidogo kidogo lakini changamoto iliyopo kwenye uwezekazaji wa kiwanda hivyo wanafanya utafuti kubaini kama wanaweza kupata samaki wa kutosha.
Mkurugenzi huyo alisema hilo linatokana na kwamba wanaopatikana kwa sasa hawatoshelezi kuendesha kiwanda ndio maana bado wawekezaji wanasita kuwekeza huko lakini kikubwa maboresha yanayoendelea kufanywa na serikali ni ya muhimu kwa sababu yatawezesha upatikanaji wa samaki kwa wingi kama uvuvi utakaofanyia utazingatia sheria za uvuvi.
Alisema jambo hilo litakuwa na tija kwao na wafanyabiashara huku akieleza kikubwa kinachowathiri wakati kunapotokea uvuvi haramu wanaua samaki ambao hawastahili kwenda sokoni matokeo yake viwanda havipati mzigo wa kutosha.
Mwisho.
Post A Comment: