Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia
wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri Mkoani Pwani, Machi
29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Askofu wa Jimbo la Ifakra, Salutarisi Libena baada ya kuweka jiwe la msingi la Shule ya Sekondari ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo iliyopo Ikwiriri mkoani Pwani, Machi 29, 2019. Katikati ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema utoaji wa elimu bora kwa Watanzania ni
moja ya vipaumbele vya nchi katika kuleta maendeleo na kufikia malengo
ya Milenia 2025, Elimu kwa wote (EFA) na Mkakati wa Kupambana na
Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA).
Amesema
ili kuweza kufanikisha malengo hayo wanahitaji sekta hiyo kuwa bora,
imara, inayokidhi mahitaji ya jamii kwa kuwapa vijana maarifa na ujuzi
wa kukabiliana na matatizo ya kijamii, kitaifa na kimataifa.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 29, 2019) wakati akiweka jiwe la
msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Parokia ya
Ikwiriri, mkoani Pwani. Ameipongeza Parokia hiyo kwa kubuni mradi wa
ujenzi wa shule.
Amesema
sekta ya elimu ni wakala wa mabadiliko katika jamii kiuchumi,
kiteknolojia na kiutamaduni katika kuleta maendeleo ya nchi na wadau
muhimu wa sekta hiyo ni pamoja na Serikali, washirika wa maendeleo,
mashirika ya kiraia na ya kidini, sekta binafsi na jamii kwa ujumla.
Waziri
Mkuu amesema kuwa wadau wote hao wamekuwa wakichangia kwa njia
mbalimbali katika kuboresha utendaji wa sekta hiyo na kusababisha
Serikali kupata mafanikio makubwa sana katika upatikanaji wa huduma za Jamii zikiwemo za elimu, afya na maji.
”Hivi
sasa kila Kijiji nchini kina shule ya msingi na ongezeko limefikia
idadi ya shule 17,659 zikiwemo zilizo chini ya Kanisa katoliki 204. Pia
tumeweza kujenga shule za sekondari katika kila kata ambapo ongezeko
limefikia shule za sekondari 4,883 nchi nzima zikiwemo zilizo chini ya
kanisa katoliki 266”.
Waziri
Mkuu amesema idadi hiyo ya shule imesaidia kutoa fursa kwa wanafunzi
wengi kupata elimu nchini katika ngazi mbalimbali. ”Hivi sasa kwa
kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2015/2010
tunatekeleza mpango wa elimu bila ada kwa kutoa sh. Bilioni 24.4 kila
mwezi”.
Amesema
lengo la Serikali la kutoa kiasi hicho cha fedha kila mwezi ni
kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule anapata fursa bila
vikwazo na Wilaya ya Rufiji nayo inanufaika, ambapo imetengewa kiasi
cha milioni 394.5 kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Lengo
la Serikali kutoa Elimumsingi Bila Ada ni kuleta ujumuishi kwa
kuhakikisha watoto wote hususan wale ambao wanatoka katika familia
zisizo na uwezo wanapata haki ya msingi ya kupata elimu.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema kuongezeka kwa ufaulu wa darasa la saba kumeleta
changamoto ya uwepo wa miundombinu ya shule za sekondari hususan kwa
kidato cha kwanza ambayo ni kielelezo cha mafanikio ya utekelezaji wa
sera ya Elimumsingi Bila Ada.
Awali, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengoalitumia fursa hiyo kuishikuru Serikalikwa kurejesha hali ya usalama na utulivu katika eneo la Rufiji na Kibiti.
Kardinali
Pengoalisema kurejea kwa hali ya utulivu na usalama katika maeneo
hayo kumemuondolea mzigo wa kiutendaji uliokuwa ukimuumiza kwa kuwa
mapadri aliokuwa akiwapangia katika parokia za huko walikuwa wakisema
‘tumekosa nini’.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, MACHI 29, 2019.
Post A Comment: