Mkurugenzi wa Clouds Media Group Ndugu Joseph kusaga ametoa ratiba ya mazishi ya mtangazaji wa Clouds FM Ephraim Kibonde aliyefariki alfajiri ya kuamkia leo jijini Mwanza.
Kusaga amesema kuwa mwili wa marehemu utawasili na kupokelewa leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere saa nne usiku na baada ya hapo utapelekwa katika hospitali ya Jeshi Lugalo kwa ajili ya kupumzishwa.
Vilevile amesema amesema taratibu za mazishi na maombolezo zitafanyika nyumbani kwake Mbezi na siku ya jumamosi ataagwa rasmi na kuzikwa.
Mtangazaji huyo amefariki leo akiwa Mwanza, baada ya kusumbuliwa na Presha toka Bukoba kwenye msiba wa Ruge Mutahaba na kuhamishiwa Mwanza. Kifo cha mtangazaji huyo kinakuja siku chache baada kufariki Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media,Ruge Mutahaba.
Post A Comment: