Na Enock Magali Dodoma.
Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) imewataka watumiaji wa mitandao kutokurusha (kupost) mambo ambayo yatapelekea kuleta athari kwa mtu binafsi au Taifa kwa ujumla
Aidha imesema uwa inachukua jitihada ya kutoa elimu kwa umma katika kuhakikisha kuwa inadhibiti mambo mbalimbali ikiwemo picha zisizofaa zinazorushwa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya Internrt nchini
Hayo yameelezwa na Mkuu wa TCRA kanda ya kati Dodoma Antonio Manyanda pindi walipoitembelea Shule ya Sekondari ya wasichana ya Kondoa iliyopo Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma kwa lengo la kutoa elimu katika kuadhimisha siku ya haki za watumiaji wa huduma Duniani
“Tunajitahidi kuwaelimisha umma ili waelewe kwamba uwanja wa Internet au Mitandao ni uwanja ambao sio salama sana na mtu asifanye mambo kwenye mitandao akadhani yuko salama,hapana”Alisema
Boniface Ngela ni afisa TEHAMA kutoka TCRA kanda ya kati Dodoma yeye amezungumzia Changamoto wananzo zipata kutokana na baadhi ya watu kurusha picha zisizofaa katika mitandao mbalimbali ya kiijamii kuwa ni kutokana na baadhi yao kutokuwa na uelewa na hiyo ndiyo sababu inayowapelekea kuendelea kutoa elimu kwa umma
“Watu wengi sana hawana uelewa hivyo basi ndio maana tupo hapa katika kutoa elimu hasa kwa hawa mabinti zetu ambao tunaamini kuwa kesho na kesho kutwa wao ndio watakuwa watumiaji wakubwa wa hii mitandao na wataweza kuitumia kwa manufaa hivyo ni bora tukawaelekeza ni nini cha wafanye na nini hawapaswi kufanya ili waweze kuitumia kwa ufasaha kwa ajili ya manufaa yao,jamii na Taifa zima kwa ujumla”Alisema
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Flora Nusu yeye amewapongeza watumishi kutoka TCRA kwa kuichagua Shule hiyo ambapo pia baadhi ya wanafunzi wamekiri kujifunza masuala lukuki yahusuyo matumizi bora ya mitandao.
Post A Comment: