Hatimaye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba umezikwa
kishujaa nyumbani kwao katika kijiji cha Kiziru Kata ya Karabagaine
Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera huku mamia ya watu wakiwemo viongozi wa
serikali wakishiriki mazishi hayo.
Zoezi la kuzika mwili wa Ruge lilianza
kwa Ibada ya mazishi ambayo iliongonzwa na Katibu wa Parokia ya Itahwa,
Anatory Kyatwa huku nyimbo za kihaya zikipamba tukio la mazishi.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga, akiweka mashada katika
kaburi la marehemu Ruge Mutahaba ambaye amezikwa leo kijijini kwao
Kiziru Bukoba.
Wazazi, familia, wakiweka mashada katika kaburi la marehemu Ruge Mutahaba ambaye amezikwa leo kijijini kwao Kiziru Bukoba.
RC Makonda akiweka shada katika Kaburi la Ruge.
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, January Makamba akiweka shada.
Awali wakati wa tukio la kuaga mwili wake katika viwanja vya Gymkhana,
Maaskofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba walimtaja Ruge kama kijana
jasiri mzalendo na mfano wa kuigwa.
Mama wa marehemu Ruge Mutahaba (wa pili kushoto), akifuatiwa na mumewe
wakiwa na aliyekuwa Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Prof.
Rwekaza Mukandala, dakika chache kabla ya mwili wa mtoto wao marehemu
Ruge Mutahaba Kuingizwa kaburini, kijijini Kiziru. Rip Ruge
Post A Comment: