Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa akisisitiza jambo wakati wa
uzinduzi wa mradi wa uendelezaji wa zao la Pamba (Cotton Victoria)
uliofanyika katika kituo cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza.
Sehemu ya washiriki wa mradi wa uendelezaji wa zao la Pamba (Cotton Victoria) uliofanyika katika kituo cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Balozi
wa Brazil nchini Tanzania Bw H.E Antonio akizungumza wakati wa uzinduzi
wa mradi wa uendelezaji wa zao la Pamba (Cotton Victoria) uliofanyika
katika kituo cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza, Kulia kwake ni
naibu Waziri wa kilimo mhe Innocent bashungwa.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa akikagua shamba la mfano wa
kilimo cha Pamba katika kituo cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza,
Jana machi 11, 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo
Tanzania na Brazil zimeingia makubaliano ya kuinua kilimo cha Pamba ili kiwe na tija kwa wakulima nchini.
Makubaliano
hayo yamejili wakati ambapo Brazil ipo katika hatua kubwa za kimageuzi
ya kilimo huku ikiwa na mafanikio makubwa katika sekta hiyo ambapo
unatekelezwa katika nchi tatu za Burundi, Kenya na Tanzania.
Mradi
wa kuinua kilimo cha Pamba unaotekelezwa na Brazil nchini Tanzania
utajikita Zaidi hasa katika kuhakikisha wakulima nchini wanapata Pamba
mbegu bora na uzinduzi wa utafiti utamfikia mkulima ili aweze kuongeza
tija.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa ameyasema hayo jana tarehe 11
Machi 2019 mara baada ya kutembelea na kukagua mashamba ya mfano wa
kilimo cha Pamba katika kituo cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza.
Mhe
Bashungwa amesisitiza kuwa serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe
Rais Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kwa kauli moja kuimarisha sekta
ya kilimo huku katika zao la Pamba imejipanga kuhakikisha inazalisha
mbegu vipara za Pamba zitakazotosheleza kwa wakulima wote nchini na kuondokana na utumiaji wa pamba manyoya ambayo imezoeleka lakini tija yake ni ndogo katika uzalishaji kuliko Pamba Manyonya.
Alisema
Wizara ya kilimo itakuwa na jukumu la kushawishi wawezaji ili kuwekeza
kwenye viwanda vya Pamba nyuzi pamoja na viwanda vya nguo na kufanya
hivyo tutakuwa tumetekeleza vyema maelekezo yaliyoainishwa kwenye ilani
ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi yam waka 2015-2020.
Aidha,
alisema kuwa Serikali pia imejipanga kupanua maabara za utafiti wa zao
la Pamba ili kuimarisha ufanisi na tija ya zao hilo kwani mafanikio ya
kilimo yanategemea zaidi katika utafiti.
Mhe
Bashungwa ameishukuru serikali ya Brazil kwa utekelezaji wa mradi huo
nchini Tanzania ambao unatokana na mahusiano mazuri katika nchi hizo
mbili inayoakisi katika kufungamanisha kilimo na uchumi wa viwanda.
Kadhalika
alisema serikali tayari imeanzisha vituo viwili vya kuzalisha Pamba
mbegu vipara katika mkoa wa Simiyu pamoja na Mkoa wa Tabora
MWISHO.
Post A Comment: