MAMLAKA ya
maji safi na usafi wa mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa inatarajiwa kuboresha
huduma ya mtandao wa maji taka kutoka asilimia 9.7 % hadi kufikia asilimia 30%
ifikapo mwaka 2030
Hayo
yamesemwa na Mkurungenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Mhandisi Geofrey Hilly wakati
wa Mkutano na waandishi wa habari wakati akitoa tathimini ya huduma za maji
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya maji nchini
Alisema kuwa
kwa kuanzia wameanza kutekeleza mradi wa uboreshaji wa mfumo wa maji taka wenye
urefu wa kilometa tatu ambao umeweza kufikia asilimia 40% na
unatarajiwa kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Alisema kuwa
mahitaji ya huduma ya maji taka ni makubwa katika Jiji hilo kwani kwa sasa
mtandao huo unapatikana katika maeneo ya kati kati ya Jiji pekee.
“Kutokana na
gharama kubwa za uwekezaji kasi ya kuongeza huduma hiyo imekuwa ni ndogo lakini
kwa mikakati iliyokuwepo watahakikisha huduma hiyo imeweza kusogeza karibu na
wananchi wengi”alisema Mkurungenzi huyo.
Hata hivyo
katika kutekeleza sera ya maji Tanga Uwasa imekuwa ikitekeleza miradi
mbalimbali ya maji katika wilaya nyingine kama vile Muheza,Pangani,Mkinga na
Kilindi.
“Katika mpango huo hakuna atakayeachwa kwani
wananchi wote wanaoishi katika eneo linalohudumiwa na mamlaka hiyo itahakikisha
wanapatiwa huduma hiyo”alisema Mhandisi hilly.
Vile vile
kwa upande wa udhibiti na uchafuzi wa vyanzo vya maji Tanga Uwasa imeweza kusaidi
upatikanaji wa huduma ya maji safi kwa vijiji vinavyozunguza chanzo cha maji
cha Mto Zigi .
“Tumefanikiwa
kupeleka mradi wa maji safi katika
vijiji vya Mashawe,Kimbo Shembekeza na vijiji jirani ambavyo vipo karibu na mto
zigi ambacho ndio chanzo cha maji”alibainisha .
Post A Comment: