1 2
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa  Jukwa la Mawasiliano ya afya kwa watu wazima(NAWEZA) kwa Mikoa ya Tabora , Arusha na Singida leo.
3
Baadhi ya viongozi na wadau mbalimbali wa sekta ya afya wakishiriki uzinduzi wa  Jukwa la Mawasiliano ya afya kwa watu wazima(NAWEZA) kwa Mikoa ya Tabora , Arusha na Singida uliofanyika leo katika Manispaa ya Tabora.
4
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungua akitoa maneno ya utangulizi wakati wa uzinduzi wa  Jukwa la Mawasiliano ya afya kwa watu wazima(NAWEZA) kwa Mikoa ya Tabora , Arusha na Singida uliofanyika leo katika Manispaa ya Tabora.
5
Meneja wa FHI Tulonge Afya Kanda Kaskazini na Kati,Dk. Benedict Kafumu akitoa maelezo mafupi kuhusu umuhimu wa   Jukwa la Mawasiliano ya afya kwa watu wazima(NAWEZA) kwa Mikoa ya Tabora , Arusha na Singida leo wakati wa uzinduzi wake ulifanyika katika Manispaa ya Tabora.
6
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Honorata Rutatanisibwa akitoa maelezo ya awali kuhusu  Jukwa la Mawasiliano ya afya kwa watu wazima(NAWEZA) leo mjini Tabora.
7
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Oscar Kapera akieleza maeneo matano yaliyomo katika  Jukwa la Mawasiliano ya afya kwa watu wazima(NAWEZA) wakati wa uzinduzi wake leo kwa ajili ya Mikoa ya Tabora, Singida na Arusha.
Picha na Tiganya Vincent
 
………………………….
NA  TIGANYA VINCENT
WADAU wametakiwa kuunganisha nguvu ili kuhakikisha kiwango cha maambukizi ya malaria Mkoani Tabora kinashuka kutoka asilimia 11 katika eneo hilo na kufikia kile cha Kitaifa cha asilimia 7.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akizundua Jukwa la Mawasiliano ya afya kwa watu wazima(NAWEZA) kwa Mikoa ya Tabora , Arusha na Singida.
Alisema hatua hiyo itafanikiwa ikiwa kutakuwepo na mawasiliano  baina ya wanajamii ili kutoa elimu sahihi itakayoasaidia kubadili tabia kwa ajili ya kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa
Mwanri alisema jitihada hizo zitasaidia kuwafanya watu wapate elimu juu ya kuangamiza mazalia ya umbu na matumizi sahihi ya vyandarua kwa ajili ya kujikinga na umbu waenezao malaria ili kuchangia malengo ya kitaifa ifikapo mwaka 2020.
Alisema kukosekana kwa taarifa sahihi zinazohusu masuala ya afya kumewafanya wananchi mkoani hapa kutumia vyandarua kufugia kuku huku wengine wakivitumia kutunzia bustani za mboga kwa kukosa elimu hivyo kushindwa kubadilika.

Mwanri alisema wanajamii ni vema wakaelimishwa juu ya kusafisha maeneo yao na kufukia madimbwi ya maji yanayozunguka nyumba zao kama hatua ya msingi ya kukabiuliana na ugonjwa wa malaria badala ya kusubiri waugue ndio elimu itolewe

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewavitaka vyombo vya habari kuisaidiana na Serikali kufikisha ujumbe sahihi kwa wananchi  ili wapate uelewa juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora itakayo wawezesha kushiriki kuinua uchumi wao na  taifa kwa ujumla.

Alisema kukosekana kwa taarifa sahihi zinazohusu masuala ya afya kumewafanya wananchi wengi kukosa elimu hiyo hivyo kushindwa kubadilika.

Kufuatia hali hiyo Mwanri alisema kuwa  vyombo vya habari vinaowajibu mkubwa wa kuhakikisha vinafikisha  elimu ya afya kwa wananchi.

Mwanri alisema kwamba wananchi wakipata taarifa sahihi kuhusu afya zao watakuwa salama na vyombo vya habari ndivyo vinaweza kufikisha kwa haraka ujumbe huo unaohusu afya zao.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa jukwaa la Naweza ni muhimu kwani linaleta uhai mpya katika akili za wananchi ili waweze kuelimika na kubadilika.

Mwanri jitihada hizo zitawezekana kama kutakuwepo na  mawasiliano ambayo yatawezesha kubadili tabia ili wananchi waweze kutumia huduma za afya sahihi na kuwa tabia chanya kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali.
Naye Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto  Oscar Kapera alisema Jukwaa la NAWEZA linalenga kufikisha ujumbe unawajengea uwezo wananchi ili waweze kubadili tabia zao za kiafya katika maeneo ya maambukizi ya VVU na mapambano dhidi ya Malaria.
Alisema maeneo mengine ni pamoja na  afya ya uzazi kwa lengo la kumwezesha mama kujifungua salama na mtoto wake kuwa salama na mapambano dhidi ya kifua kikuu.
Share To:

Post A Comment: