Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Constantine Kanyasu (wa tatu
kulia) akipewa maelezo kutoka kwa mkazi wa eneo la kihisitoria la
Mikindani, Said Halfani kuhusiana na kisima cha asili cha Haikata
kilichopo tangu mwaka 1545 ambacho hadi sasa kina maji yanayotumiwa
na wakazi wa eneo hilo wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea kwa ajilli
ya kujionea kisima hicho ambacho ni moja ya kivutio cha utali katika
eneo hilo la Mikindani mkoani Mtwara. Wenghine ni wananchi pamoja na
watumishi wa mkoa huo
Baadhi ya jengo la zamani la kihistoria la ambalo ni kivuto cha utalii ambapo Taasisi za Uhifadhi nchini zitakuwa na jukumu la kukarabati pamoja na kuyasimamia ili kuchagiza utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Constantine Kanyasu akioneshwa baadhi ya picha kutoka kwa Afisa wa Malikale a,mbaye ni mkuu wa Kituo cha Makumbusho ya Mikindani, Paul Ngahane wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea eneo la kihistoria la Mikindani liliopo katika mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kujionea maeneo ya kihistoria.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja kwenye bango la kisima cha asili cha Haikata kilichopo tangu mwaka 1545 ambapo hadi hivi sasa maji hayo yanaendelea kutumiwa na wakazi wa mji wa kihistoria wa Mikindani.
.Moja jengo la kihistoria ambalo Taasisi za uhifadhi nchini zinatarajia kukayakarabati kwa ajili ya utalii wa kiutamaduni na khistoria.
Hatua
hiyo imekuja baada ya Serikali kupitia upya sera ya Malikale ya namna
ya kuyahifadhi maeneo hayo kufuatia majengo mengi ya kale na ya
kihistoria kuwa katika hali mbaya ya uchakavu.
Baadhi ya jengo la zamani la kihistoria la ambalo ni kivuto cha utalii ambapo Taasisi za Uhifadhi nchini zitakuwa na jukumu la kukarabati pamoja na kuyasimamia ili kuchagiza utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Constantine Kanyasu akioneshwa baadhi ya picha kutoka kwa Afisa wa Malikale a,mbaye ni mkuu wa Kituo cha Makumbusho ya Mikindani, Paul Ngahane wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea eneo la kihistoria la Mikindani liliopo katika mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kujionea maeneo ya kihistoria.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja kwenye bango la kisima cha asili cha Haikata kilichopo tangu mwaka 1545 ambapo hadi hivi sasa maji hayo yanaendelea kutumiwa na wakazi wa mji wa kihistoria wa Mikindani.
.Moja jengo la kihistoria ambalo Taasisi za uhifadhi nchini zinatarajia kukayakarabati kwa ajili ya utalii wa kiutamaduni na khistoria.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Constantine Kanyasu (wa tatu
kulia) akipewa maelezo kutoka kwa mkazi wa eneo la kihisitoria la
Mikindani, Said Halfani kuhusiana na kisima cha asili cha Haikata
kilichopo tangu mwaka 1545 ambacho hadi sasa kina maji yanayotumiwa
na wakazi wa eneo hilo wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea kwa ajilli
ya kujionea kisima hicho ambacho ni moja ya kivutio cha utali katika
eneo hilo la Mikindani mkoani Mtwara. Wenghine ni wananchi pamoja na
watumishi wa mkoa huo.
Serikali
imeanza mkakati maalum wa kuinua Utalii wa kiutamaduni na wa kihistoria
kwa kuvigawa vituo 16 vya Malikale kwa Taasisi za uhifadhi nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.
Constantine Kanyasu alipotembelea mji wa kihistoria wa Mikindani katika
Manispaa ya Mikindani,mkoani Mtwara ambao kwa sasa eneo lake
linasimamiwa na kuendeshwa na Taasisi ya Makumbusho ya Taifa.
Amesema
lengo la uamuzi huo ni kuziwezesha Taasisi zitakazokuwa na jukumu la
usimamizi ziyakarabati na kuyasimamia maeneo hayo ya kihistoria ili
yaweze kuchangia katika pato la Taifa kupitia sekta ya utalii nchini.
Mhe.
Kanyasu amesema vituo hivyo 16 vitawekwa chini ya Hifadhi za
Taifa(TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro(NCAA), Mamlaka
ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA), Makumbusho ya Taifa(NMT)
pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS).
Ameeleza
kuwa Taasisi hizo zitakuwa na jukumu la kusimamia, kukarabati,
kuendeleza, kuendesha pamoja kutangaza vituo hivyo vyenye utajiri
mkubwa wa kihistoria na kiutamaduni.
Aidha,
kwa mujibu wa tathmini ya ukaguzi iliyofanyika mwaka jana jumla ya
majengo 85 ya kihistoria yalikuwa yapo hatarini kudondoka na kupotea
kabisa yasipokarabatiwa.
Kufuatia
hali hiyo Mhe. Kanyasu amesema Taasisi hizo zitasaidia kuyakarabati
majengo hayo ili yaweze kurudi katika hali yake ya mwanzo na kuwa
kichocheo cha Utalii
Akizungumzia
mkakati wa kutangaza vivutio hivyo vya Malikale amesema vitakuwa
vikitangazwa kwa mfumo wa vifurushi (packages) ili kuwawezesha watalii
wanapokwenda Mtwara waweze kutembelea vivutio vingi vilivyopo katika
mkoa huo kwa vile ni ngumu kwa mtalii kwenda Mtwara kwa ajili ya
kutembelea mji wa Mikindani pekee.
‘’Tunataka
vivutio vya utalii vya Kusini na maeneo mengine ya nchini yawekwe
kwenye vifurushi ili mtalii akipanga kwa mfano kutembelea mkoa wa
Mtwara atembelee Pori la Akiba la Lukwika Lumesule akitoka hapo
atembelee majengo ya kale, ajionee vikundi vya ngoma za asili kisha
aende akapumzike kwenye fukwe zetu nzuri’’ Amesema.
Awali
akizungumza kuhusu majengo ya Kale, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa
ya CCM wa mkoa wa Mtwara, Lukasi Elwesi amemueleza Naibu Waziri huyo
kuwa mikoa ya Kusini imejaliwa kuwa na majengo ya kale mengipamoja na
fukwe ambazo hazijaguswa hivyo, ameiomba Wizara iongeze nguvu katika
Kanda hiyo.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Malikale, Dkt. Fabian Kigadya amezitaka
Halmshauri nchini kulinda na kuendeleza majengo ya kihistoria kwa ajili
ya kuvutia watalii hali itakayosaidia kuongeza mapato ya Halmashauri
kupitia malikale hizo.
Post A Comment: