Mtangazaji wa Clouds FM, Gardner amezungumzia kifo cha rafiki yake na Mtangazaji mwenzie, Ephraim Kibonde waliyekuwa wanatangaza wote katika kipindi cha Jahazi.

Garder amesema kuwa yeye na Kibonde walikuwa na Chemistry katika Utangazaji mpaka sasa haelewe atafanyaje tena kazi bila marehemu Kibonde.

"Kiukweli kwenye utangazaji kuna kitu kinaitwa Chemistry mimi na Kibonde tulikuwa na Chemistry yeye akisema mimi nilikuwa najibu, hata sielewi ntafanyaje tena kazi bila Kibonde kwa kweli," amesema Gardner.

Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph kusaga amesema kuwa mwili wa marehemu utawasili na kupokelewa leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere saa nne usiku na baada ya hapo utapelekwa katika hospitali ya Jeshi Lugalo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: