Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kamati ya kudumu ya bunge ya Ardhi ,Maliasili na Utalii iliyotembelea hifadhi hiyo ili kujionea mradi wa Faru unavyotekelezwa.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Profesa Dos Santos Silayo akizungumza wakati wa ziara hiyo
Kaimu Mkurungenzi Mkuu wa hifadhi ya taifa nchini TANAPA Martin Loibooki kulia akimueleza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu namna wanavyotekeleza mradi wa kuhifadhi faru kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi,Maliasili na Utalii Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto(CCM)

MKURUGENZI Usimamizi wa Rasilimali za Misitu na Nyuki nchini Zawadi Mbwambo akiwaonyesha kitu wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii

   Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakiwa kwenye gari maalumu kwenye hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ambapo walitembelea
ili kujionea mradi wa Faru unavyotekelezwa.
Sehemu ya wajumbe wa kamati hiyo wakiwa ndani ya ofisi ya Hifadhi ya Asili ya Misitu ya Chome wilayani Same mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yao
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu kulia akiteta jambo na Kaimu Mkurungenzi Mkuu wa hifadhi ya taifa nchini TANAPA Martin Loibooki wakati wa ziara hiyo
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi,Maliasili na Utalii Shabani Shekilindi alimaaru Bosnia akiwa na wajumbe wa kamati hiyo wakitoka ofisi za Msitu wa Hifadhi ya Chome wilayani Same mkoani Kilimanjaro


SERIKALI imesema inakusudia kuifanya Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi kuwa ndio eneo maalum la kukuzia na kuzalishia wanyamapori aina ya Faru kisha kuwapeleke maeneo mengine kwa ajili ya kuendelea na maisha yao.


Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu wakati wa ziara ya kamati ya kudumu ya bunge ya Ardhi ,Maliasili na Utalii iliyotembelea hifadhi hiyo ili kujionea mradi wa Faru unavyotekelezwa.

Alisema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wanaongeza wingi wa wanyama hao kwa kuongeza uzalishaji wao kisha kuwapeleka katika maeneo mengine.

“Kwa sababu faru walikuwa wanakaribia kutoweka hivyo tumeamua kutenga eneo maalum ili kuongeza uzalishaji wao na serikali kuendele kupata mapato kutoka na utalii wa wanyama hao katika maeneo mengine”alisema Naibu Waziri huyo.


Hata hivyo alisema kuwa sasa hivi hifadhi ya Mkomazi wanajenga eneo jingine maalum kwa ajili ya kufanya utalii wa faru wachache tofauti na eneo lile ambalo wanazalishwa.

Nae Kaimu Mkurungenzi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa nchini TANAPA Martin Loibooki alisema kuwa kazi kubwa inayofanyika katika eneo hilo ni uzalishaji wa faru weusi.

Alisema kuwa kupitia mradi huo mafanikio yameanza kuonekana kwani wanyama hao wameweza kuongezeka kwa wingi tofauti na hapo awali.

Awali Mratibu wa Mfuko wa Kimataifa wa mradi wa uhifadhi wa wanayamapori Lucy Tonny alisema kuwa wanaishukuru serikali ya Tanzania kwa hatua waliyoichukuwa ya kuhakikisha wanaongeza kizazi cha wanayaka hao ambao walikuwa hatarini kutoweka.

Alisema kuwa kwa kushirikina na serikali wataweza kuhakikisha wanaongeza uzao wa wanyama hao kwa maendeleo endelevu.

“Ni mradi wa siku nyingi lakini tunashukuru namna ambavyo serikali ilivyojitahidi kuwekeza nguvu kubwa katika hilo kwa vitendo”alisema Tonny.

MWISHO
Share To:

Post A Comment: