Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (aliyevaa Kapelo) akiongoza
ukaguzi wa ujenzi wa madarasa manane yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi
na michango ya wadau katika shule ya Msingi Msia, kata ya Milepa
Wilayani Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akipewa maelezo juu ya marekebisho yanayoendelea katika ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Msia na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Mh. Kalolo Ntila (kaunda suti nyeusi) wakati wa kuyakagua madarasa hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akichanganya mchanga na saruji wakati ujenzi wa madarsa ya shule ya sekondari Msia ukiendelea.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akichanganya mchanga na saruji wakati ujenzi wa madarsa ya shule ya sekondari Msia ukiendelea
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akipewa maelezo juu ya marekebisho yanayoendelea katika ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Msia na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Mh. Kalolo Ntila (kaunda suti nyeusi) wakati wa kuyakagua madarasa hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akichanganya mchanga na saruji wakati ujenzi wa madarsa ya shule ya sekondari Msia ukiendelea.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akichanganya mchanga na saruji wakati ujenzi wa madarsa ya shule ya sekondari Msia ukiendelea
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Mh. Joachim Wangabo ameliagiza jeshi la polisi Mkoani Humo kuhakikisha
wanamsaka na kumkamata mganga wa jadi anayesadikiwa kuwaibua na kuwaadhiri
wachawi katika bonde la ziwa Rukwa Wilayani Sumbawanga.
Agizo hilo limekuja
baada ya kufanya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali katika bonde hilo
pamoja na kujionea maendeleo na changamoto za shule ya sekondari Kipeta iliyoezuliwa
paa pamoja na shule ya msingi Msia iliyobomoka madarasa manne kutokana na mvua
iliyoambatana na upepo mkali iliyosababisha madhara hayo mwezi Disemba mwaka
2018.
Ameonya kuwa hataki
yaliyotokea mkoa wa Njombe yajirejee katika Mkoa wa Rukwa ikiwa bado watu
hawajasahau machungu waliyoyapata kutokana na matukio hayo, na kuongeza kuwa
mganga huyo wa kienyeji analindwa na kiongozi wa chama cha kisiasa na hivyo
kumtaka mkuu wa kituo cha Kijiji cha Kilyamatundu kuhakikisha anamkamta
kiongozi huyo hata kama ni wa Chama cha Mapinduzi.
“OCS na vyombo vyako
vile fanya upepelezi wa kina na ukamate yeyote yule ambae ametoka nje ya mkoa
huu, nje ya Kilyamatundu anayefanya shughuli hizi, kamata weka ndani fanya
mahojiano ya kina, na wengine nimeambiwa hap ani viongozi wa vyama vya kisiasa,
usijali huyu ni chama tawala, huyu ni nani, kama ukijua kwa uhakika kamata mhoji
mpaka kieleweke, sisi hatutaki kuletewa Lambalamba hapa,” Alisisitiza.
Katika hatua nyingine, Mh.
Wangabo aliwapongeza waalimu, Uongozi wa vijiji husika pamoja na wananchi kwa ushirikiano
waliouonyesha katika kuhakikisha majengo yaliyobomoka na kuezuliwa katika shule
hizo yanarudi katika hali yake ya kawaida na hatimae wanafunzi kuendela na
masomo.
Pamoja na michango ya wadau
mbalimbali iliyohamasishwa na Mh. Wangabo ambayo imesaidia kurudishisa mapaa ya
majengo ya utawala, mabweni mawili, nyumba sita za waalimu na vyoo vya
wasichana na wavulana kwa shule ya sekondari Kipeta na kujenga madarasa manane
kwa shule shule ya Msingi Msia, Wizara ya Elimu pamoja kwa ushirikiano na
Wizara ya TAMISEMI imetoa shilingi Milinoni 75.2 kwaajili ya kuongezea ujenzi
wa madarasa na vyoo kwa shule hizo.
Naye Diwani wa kata ya
Milepa Mh. Apolinari Macheta alipongeza juhudi za Mkuu wa Mkoa kwa kuhakikisha
shule hizo zinakuwa bora zaidi ya zilivyokuwa na kumuahidi kuwa Shilingi
Milioni 48.6 walizopatiwa kwaajili ya ujenzi wa madarasa mawili na vyoo matundu
sita kwa shule ya msingi Msia atahakikisha kwa ushirikiano wa wananchi watapata
darasa jingine kwa fedha hizo.
Post A Comment: