Mkuu wa Mkoa wa Songwe  Brigedia Generali Mstaafu Nicodemaswa pili kushoto akiteta jambo wakati alipokwenda kukagua  maandalizi hayo
 Mkuu wa Mkoa wa Songwe  Brigedia Generali Mstaafu Nicodemaswa kushoto akionyeshwa maeneo mbalimbali


IKIWA zimebaki takribani wiki mbili ili Mwenge wa Uhuru uwashwe tukio ambalo litafanyika April 2 mwaka huu Mkoani Songwe Mkuu wa Mkoa huo Brigedia Generali Mstaafu Nicodemas Mwangela ametembelea eneo kutakapowasha na kukagua maandalizi yake .

Akizungumza mara baada ya kukagua maandalizi hayo aliwataka  wananchi wa mkoa wa songwe kujitokeza kwa wingi katika kuupokea na kuchamgamkia fursa za biashara ambapo amesema watakaopewa kipaumbele ya kufanyabiashara ni wale ambao wanavitambulisho vya mjasiliamali.

Nao wananchi wa mkoa wa songwe wamesema ujio wa mbio za mwenge kitaifa wanaomba ulete hamasa katika miradi ya maendeleo ambayo haijatekelezwa ama kutokamilika na kusababisha Kero ya kudumu.

Aidha RC  Mwangela  amesema katika uzinduzi wa mbio za mwenge kutakuwa na michezo mbalimbali ambayoitatangulia week moja kabla ya tukio hilo la uzinduzi hivyo baadhi ya wasanii wakakuwepo katika tukio hilo....


Mwisho

Share To:

Post A Comment: