Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti amesema kuwa Ugonjwa wa Ukimwi
umekaa mahali pabaya na hakuna Jeshi la kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi (VVU) zaidi ya jamii kujitunza wenyewe.
Mkuu huyo ameyasema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara kwenye uzinduzi wa Kituo cha kutolea huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (CTC) Mirerani.
Mnyeti alisema hakuna jeshi la kuzuia Ugonjwa huo japokuwa maambukizi ya VVU kwenye mkoa wake siyo mengi sana hivyo Wananchi waendelee kujikinga na maambukizi mapya.
Mnyeti alisema mji mdogo wa Mirerani ndiyo sehemu inayoongoza kwenye mkoa huo kwa kuwa na watu wengi wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Pia alisema maambukizi ya VVU kwa mkoa wa Manyara ni asilimia 2.3 na kwenye mji mdogo wa Mirerani ni asilimia 16 hivyo eneo hilo pekee ndilo linasababisha mkoa huo uwe na asilimia hiyo.
Post A Comment: