Mbunge wa Babati Vijijini, Vrajlal Jituson amejikuta akikemewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti na kuambiwa kuwa atachukuliwa hatua kwa kile alichodaiwa kuwa anahamasisha vitendo vya uvunjifu wa sheria.

Vrajlal Jituson amejikuta kwenye hali hiyo wakati wa mkutano wa hadhara uliyomuhisisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti na baadhi ya wafugaji kwa ajili ya kutatua mgogoro wa ukamatwaji wa ng'ombe wa baadhi ya wafugaji hao.

Akizungumza kwenye mkutano, Mnyeti amesema kuwa, “nataka nikwambie mbunge kwamba nakuheshimu sana, sitaki uendelee kuchochea migogoro, na mimi mtu akivunja sheria simkamati aliyevunja, namkamata aliyemtuma kuvunja, sitaki mtu aje kunipapasa sharubu,”

“Anakuja mwanasiasa kwa njaa ya kura za mwakani anadanganya watu halafu wakipigana na kuuana anakimbilia Dodoma hilo sitalikubali litokee Manyara,” ameongeza Mnyeti.

Hata hivyo, Jituson alikanusha madai hayo ya uchochezi na kueleza kuwa hakuwahi kufanya hivyo.

Alisema migogoro ya ardhi katika jimbo la Babati Vijijini ilikuwapo miaka mingi hata kabla hajawa mbunge na eneo hilo lina mgogoro wa zaidi ya miaka 10.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: