Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amepanga
kukutana na makundi ya watu mbalimbali ikiwemo wahudumu wa Bar, Hotel,
wafanyakazi wa Saloon na wafanyakazi wa nyumbani kwa lengo la
kusikiliza kero na malalamiko yao baada ya kubaini wengi wao wamekuwa
wakifanyiwa vitendo vya udhalilishaji na unyanyasaji ikiwemo kutolewa
lugha za matusi kutoka kwa baadhi ya *wanaume wasiojiheshimu.
RC Makonda amesema kuwa katika mkutano wake na makundi
hayo atataka kufahamu masuala ya mishahara, ajira,changamoto
wanazopitia na suala zima la usalama wanaporudi majumbani usiku wa
manane ambpo ameeleza kuwa anachokitaka ni kuona kila mtu anaheshimu
kazi ya mwenzake.
Hayo yote yamejiri leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya wanawake yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City.
Post A Comment: