MKUU
wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi leo amezindua Jukwaa litakaloshughulikia
maswala ya Afya kwa Watu wazima hususani Afya ya Mama na Mtoto Mkoani
Iringa.
NAWEZA
ni Jukwaa linalolenga kufikisha elimu sahihi itakayowajengea uwezo
wananchi wabadili tabia na mitizamo hasi ili kuleta matokeo chanya ya
kiafya. Akizindua jukwaa hilo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ali Hapi alisema
lengo la serikali ni kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga
vinavyosababishwa na changamoto mbalimbali zikiwemo huduma duni na
ukosefu wa elimu na matumizi sahihi ya huduma za afya na afya ya uzazi.
Alisema
kuwa serikali kwa kushirikiana na mradi wa USAID Tulonge Afya fhi 360
inajitahidi kuelimisha jamii juu ya afya ya uzazi katika kupunguza vifo
vya wajawazito wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua, vifo vya
watoto wachanga lakini pia vifo vinavyotokana na ugonjwa wa malaria.
Mkuu
huyo wa mkoa alisema kuwa vyombo vya habari vina jukumu kubwa la
kuisaidia serikali kwa kufikisha ujumbe na elimu sahihi kwa wananchi na
jamii wapate uelewa na umuhimu wa kuwa na afya bora itakayowawezesha
kushiriki shughuli za uzalishaji na kuinua uchumi wao.
Kwa
mujibu wa Hapi jukwaa hilo litatoa huduma jumuishi za afya katika
maeneo ya afya ili kuiwezesha serikali kufanikisha mikakati na
vipaumbele vyake vya kupunguza maambukizi ya Ukimwi (VVU), vifo vya
akina mama vitokanavyo na uzazi,vifo vya watoto wachanga, malaria na
kifua kikuu (TB).
Aidha,
alisema kukosekana kwa taarifa sahihi za masuala ya afya kumesababisha
wananchi wengi wakose elimu sahihi ya matumizi ya afya ya uzazi na
hivyo kushindwa kubadili tabia zao kiafya.
"Takwimu
zinaonyesha kuwa vifo vya akina mama 556 hupoteza maisha kila mwaka
kati ya vizazi hai 100,000 huku watoto wakiwa 25 kati ya 1,000 nao
wakifariki baada ya kuzaliwa, hivyo serikali inataka hali ibadilike
ifikapo 2020,"alisema Hapi na kuongeza kuwa nia ya serikali ni kuonavifo
vya wajawazito vinapungua hadi kufikia 292 na watoto chini ya miaka 5
vishuke na kufikia 16 kwa mwaka.
Hata
hivyo asilimia 25 ya kina mama ndio wanaokwenda kliniki baada ya
kupata ujauzito, huku 63 asilimia wakijifungulia vituo vya afya hivyo
NAWEZA inalenga kuwasaidia katika changamoto za maradhi na ujauzito.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akizungumza na wadau wa Afya wa Mkoa wa
Iringa (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua Jukwaa la “NAWEZA”
litakalozungumzia maswala ya Afya kwa watu wazima hususani Afya ya Mama
na Mtoto.Uzinduzi huo umefanyika leo Mkoanim humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi (kushoto) na Mwakilishi kutoka USAID,
Ananthy Thambinayagamwa wakipiga makofi mara baada ya Mkuu wa Mkoa
kuzindua Jukwaa la “NAWEZA” litakalozungumzi maswala ya Afya kwa watu
wazima hususani Afya ya Mama na Mtoto.Uzinduzi huo umefanyika leo
Mkoanim humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau
mbalimbali mara baada ya kuzindua Jukwaa la “NAWEZA” litakalozungumzi
maswala ya Afya kwa watu wazima hususani Afya ya Mama na Mtoto.Kulia ni
Mwakilishi kutoka USAID Tulonge Afya, Jacqueline Larsen, Mkuu wa Wilaya
ya Iringa, Richard Kasesela na Mwakilishi kutoka USAID, Ananthy
Thambiayagam.Uzinduzi huo umefanyika leo Mkoani humo.
Post A Comment: