Wakati leo wachezaji wa Taifa Stars wameitwa Ikulu Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemuomba radhi Rais John Magufuli suala la nusu bei.
Utakumbuka Wiki iliyopita RC Makonda alitangaza kuwa iwapo Taifa Stars itawafunga Uganda na kufuzu AFCON, basi vinywaji vyote Jijini Dar es Salaam vitauzwa nusu bei kwa saa sita na hilo likafanyika.
"Rais naomba radhi kwa tukio la jana watu wamelewa sana na nina uhakika kuna uwezekano watu hawajafika Maofisini, nitumie fursa hii kuomba radhi Maboss wote ndani ya DSM, hali ilikuwa sio hali nakuahidi Rais sitorudia hiki kitendo cha nusu bei," amesema RC Makonda.
Hapo jana Taifa Stars ilishinda goli 3-0 dhidi ya Uganda na kukata tiketi ya kufuzu kucheza Fainali ya Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika nchini Misri mwaka huu.
Post A Comment: