Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Kiongozi wa Ujumbe kutoka nchini Morocco Balozi Mohamed
Methqal ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Ushirikiano wa Kimataifa
wa Morocco mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. katikati
ni Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane akishuhudia.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika kikao na Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane ambaye
aliambatana pamoja na Kiongozi wa Ujumbe kutoka nchini Morocco Balozi
Mohamed Methqal ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Ushirikiano wa
Kimataifa wa Morocco, Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha
ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa
Palamagamba Kabudi, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini Patrick
Mfugale pamoja na wajumbe wengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza jambo kuhusu ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu utakaokuwa
na uwezo wa kuingiza watazamaji zaidi ya 85,000 mkoani Dodoma huku
Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah Benryane wanne kutoka (kushoto)
pamoja na Kiongozi wa Ujumbe kutoka nchini Morocco Balozi Mohamed
Methqal watatu kutoka kushoto pamoja na ujumbe huo wakisikiliza.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia
mfano wa Uwanja mkubwa wa mpira wa miguu utakaojengwa jijini kwa
ufadhili wa Mfalme wa Morocco Mohamed VI. Uwanja huo utakuwa na uwezo
wa kuchukua watazamaji 85,000 (normal capacity) waliokaa kwenye viti
lakini pia utaweza kubeba washabiki hadi105,000 kama walivyopanga. Kwa
nje uwanja huo utakuwa na muonekano kama mlima Kilimanjaro hivyo kuzidi
kupamba madhari ya mjii mkuu wa Tanzania mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Balozi wa Morocco hapa nchini Abdelilah
Benryane wasabi kutoka kushoto akifatiwa na Kiongozi wa Ujumbe kutoka
nchini Morocco Balozi Mohamed Methqal ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa
Wakala wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Morocco pamoja na Ujumbe wao.
Wengine katika picha ni ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi wasabi kutoka kulia,
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Patrick
Mfugale wasita kutoka kulia, Balozi Zuhuru Bundala wakwanza kulia
pamoja na wajumbe wengine Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Post A Comment: