Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa amesema haoni umuhimu wa maadhimisho ya wiki ya maji ilhali wananchi wanalalamikia ukosefu wa maji, hivyo kutaka hatua stahiki zichukuliwe ili malengo ya kumpatia kila mwananchi maji safi na salama yatimie.

Waziri Mbarawa amesema hayo jijini Dodoma wakati akizindua ripoti za utendaji wa mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira zilizowasilishwa na Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na Maji EWURA.

Akizungumza na watendaji kutoka mamlaka mbalimbali za maji nchini pamoja na watendaji wa EWURA waziri Mbarawa anasema haoni umuhimu wa watendaji hao kupongezana ikiwa bado kuna vilio vya ukosefu wa maji maeneo mbalimbali ya nchi.

Huku pia akiitaka EWURA ambayo ndiyo yenye wajibu wa kuratibu, kusimamia na kukuza sekta ya maji na nishati nchini kuangalia bei za maji maeneo ya vijijini kwani ni kubwa kulinganisha na maeneo ya mjini
Share To:

msumbanews

Post A Comment: