Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi Bi. Khadija
Mwenda akieleza umuhimu wa kuzingatia kanuni za kutoa huduma ya kwanza kwa
mgonjwa au mtu aliyepata ajali wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Katiba na Sheria Machi 27, 2019 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Tafiti na Takwimu kutoka Wakala wa Afya na Usalama mahala pa Kazi (OSHA) Bw. Joshua Matiko akiwasilisha mada wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wabunge ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuongeza tija.

Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakifuatilia semina ya kuwajengea uwezo kuhusu majukumu ya OSHA leo jijini Dodoma.

Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. David Mathayo akichangia jambo
wakati wa mafunzo hayo.
(PICHA
ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
|
NA;
MWANDISHI WETU
Wakala wa Afya na Usalama Mahala
Pa Kazi umepongezwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa
kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi ili kusaidia nguvu kazi iliyopo
kutumika kuchochea maendeleo.
Akizungumza wakati wa
semina kwa wabunge wa Kamati hiyo iliyofanyika Machi 27, 2019 katika Bungeni
Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Mohamed Mchengelwa amesema kuwa Wakala huo umeonesha mfano bora katika
kutekeleza majukumu yake na pia kwa kuwajengea uwezo wabunge kuhusu masuala ya usalama mahala pa kazi na umuhimu
wake katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
“Elimu tuliyopata ni muhimu kwetu na kwa
wananchi hivyo pamoja na kazi nzuri mnayofanya ni vyema sasa elimu hii
ikatolewa kwa wananchi wote na wabunge kwa ujumla ili kusaidia kupunguza athari
zinazotokana na kukosekana kwa elimu kuhusiana na masuala ya Usalama Mahali Pa
Kazi ikiwemo namna ya kutoa huduma ya kwanza,” alisisitiza Mchengelwa
Akifafanua amesema kuwa
katika masuala ambayo Kamati hiyo imetoa ni pamoja na kuongeza kiwango cha
utoaji wa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari.
Kwa upande wake Naibu
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana Mhe.
Antony Mavunde amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa wabunge
wanapata uelewa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya OSHA.
Aliongeza kuwa kuna umuhimu
mkubwa wakuwajengea uwezo wabunge kama wawakilishi wa wananchi ili waweze
kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
“Lengo letu kama Serikali
ni kuhakikisha kuwa tunalinda nguvu kazi iliyopo ili iweze kusadia katika
ujenzi wa uchumi wa viwanda na maendeleo ya Taifa kwa ujumla,” alisisitiza
Mavunde
Kwa upande wake Kaimu
Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi. Khadija Mwenda amesema kuwa wameandaa semina hiyo kwa
wabunge ili kuwajengea uwezo wa kujikinga na athari za ajali au panapotokea
mgonjwa anayehitaji kupata msaada wa huduma ya kwanza katika mazingira yao ya
kazi na mengine yanayowazunguka.
Aliongezea kuwa OSHA
itaendelea kutoa elimu kwa umma ili kujua namna bora za kujilinda na kujiepusha
na madhara yanayoweza kuwapata wawapo kazini pamoja na mazingira yote
yanayowazunguka kwa kuzingatia misingi ya elimu ya utoaji wa huduma ya kwanza
endapo kunatokea dharula au majanga kazini.
“Tumejipanga kuwafikia
watanzania kwa wingi wao ili kutoa elimu kwa umma juu ya masuala ya Usalama
mahala Pa Kazi kwa kuzingatia unyeti wa masuala hayo kwani ni muhimu wananchi
wakaelewa namna bora za kujilinda kuepuka madhara wawapo kazini,”alisema
Bi.Mwenda
OSHA imekuwa ikiwajengea
uwezo makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo wabunge na wananchi ili waweze
kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuilinda nguvu kazi iliyopo kwa maslahi
mapana ya Taifa letu.
=MWISHO=
Post A Comment: