Mbunge
wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe
Japhet Hasunga akishiriki shughuli za maendeleo pamoja na wananchi
wakichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika
shule ya msingi Masangula iliyopo katika kata ya Nyimbili akiwa katika
ziara ya ukaguzi na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimboni
Vwawa. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Mbunge
wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe
Japhet Hasunga akikagua shamba la Kahawa lenye ukubwa wa zaidi ya Hekari
400 linalomilikiwa na Diwani wa Kata ya Nyimbili Mhe Tinson Nzunda
wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi na utekelezaji wa ilani ya Chama
Cha Mapinduzi Jimboni Vwawa.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza kwenye ibada maalumu ambapo
alichangia Shilingi 1,000,000 kwa ajili ya uendelezaji wa shughuli za
ufugaji nyuki katika vikundi vya ufugaji nyuki kwenye kanisa la FPCT
Ilolo sambamba na kuchangia kwaya kwa ajili ya kuendelea kuhubiri
injili.
Mbunge
wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe
Japhet Hasunga akicheza ngoma ya asili pamoja na wananchi akiwa katika
ziara ya ukaguzi na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimboni
Vwawa.
Mbunge
wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe
Japhet Hasunga akisalimiana na wazee akiwa katika ziara ya ukaguzi na
utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimboni Vwawa.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Wakala
wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umetakiwa kununua mahindi mengi
kwa wakulima kwani kufanya hivyo kutaongeza wigo wa masoko kwa wakulima
wa mazao mbalimbali ya nafaka nchini.
Mbunge
wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe
Japhet Hasunga ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Wasa vilevile katika kijiji
cha Ibebwa kilichopo katika kata ya Msia akiwa katika ziara jimboni
humo kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye miradi
ya maendeleo.
Mhe
Hasunga alisema kuwa NFRA inapaswa kubadili dhana ya kununua mahindi
kwa ajili ya hifadhi pekee badala yake wanapaswa kununua mahindi kwa
ajili ya kuyauza ili kuongeza ufanisi wa soko kwa wakulima nchini.
Katika
hatua nyingine alisema kuwa tayari NFRA imeanza kutekeleza maelekezo ya
serikali kwa kununua na kuuza mahindi kupitia mkataba na Mpango wa
Chakula Duniani (WFP) utakaopelekea kurejea sokoni kununua mahindi kwa
wakulima.
Alisema NFRA pamoja na Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko zinapaswa kutekeleza wajibu wake katika ufanyaji biashara ya mazao.
Pamoja
na mambo mengine Mhe Hasunga ameshiriki shughuli za Maendeleo ikiwemo
ujenzi wa shule ya Sekondari Msia sambamba na ujenzi wa vyumba viwili
vya madarasa, nyumba moja ya mwalimu na matundu sita ya vyoo katika
shule ya msingi Masangula iliyopo katika kata ya Nyimbili.
Vilevile
akiwa katika ibada maalumu kwenye kanisa la FPCT Ilolo amemuagiza
Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri ya Wilaya ya Mbozi kuhakikisha kuwa
vikundi mbalimbali vya ufugaji nyuki vinasajiliwa.
Aidha,
alichangia jumla ya Shilingi 1,000,000 kwa ajili ya uendelezaji wa
shughuli za ufugaji nyuki katika vikundi vya ufugaji nyuki kwenye kanisa
la FPCT Ilolo sambamba na kuchangia kwaya kwa ajili ya kuendelea
kuhubiri injili.
Aliongeza
kuwa watanzania wanapaswa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya
tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kufanya kazi
kwa bidii huku akisisitiza kuishi katika matendo mema na kutobaguana
katika shughuli za Maendeleo.
Kuhusu
changamoto za upungufu wa walimu katika shule mbalimbali Waziri Hasunga
alisema kuwa serikali imejipanga kutatua changamoto hizo na kwa kuanza
tayari imetoa kibali cha kuajiri waalimu zaidi ya 4000 huku juhudi
zingine ikiwa ni pamoja na kuwahamisha walimu kwenye shule ambazo zina
walimu wa ziada.
Post A Comment: