Mkurugenzi Mtendaji wa TOTAL Tanzania Tarik Moudaffal akizungumza wakati wa halfa hiyo
 Mkurugenzi Mtendaji wa TOTAL Tanzania Tarik Moudaffal kushoto akiwa na Naibu Waziri wa Naibu Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde kulia
  Naibu Waziri wa Naibu Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde kulia akikabidhi hundi kwa washindi wa andiko

Naibu Waziri wa Naibu Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde kulia akimkabidhi cheti na tunzo mmoja wa washindi wa shindano la andiko la Mradi lililofadhiliwa na kampuni ya TOTAL

 
Naibu Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde ametoa rai kwa sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kuwajengea ujuzi Vijana wa Tanzania kupitia Program mbalimbali za kukuza ujuzi ili kuwajengea uwezo na sifa za kuajirika ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa  na Mavunde katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam wakati wa kukabidhi tuzo kwa washindi wa Shindano la andiko la Mradi lililofadhiliwa na Kampuni ya (TOTAL),ambapo alitumia fursa hiyo kuipongeza kampuni ya hiyo kwa kuwawezesha Vijana kuongeza mtaji na pia kwa kusaini makubaliano na Chuo kikuu Dar es salaam(UDSM) kuchukua wanachuo 20 kwa ajili ya kuwapatia mafunzo na kuwapatia uzoefu katika fani mbalimbali.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mkurugenzi Mtendaji wa TOTAL Tanzania Tarik Moudaffal amesema kwamba kila mwaka kampuni yake hushindanisha Vijana wenye andiko la mradi ambapo huwawezesha kiasi cha fedha kwa ajili ya kutekeleza wazo Biashara hilo ikiwa ni pamoja na kuwalea kupitia viaatamizi (Incubator) nchini Ufaransa kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi.

Katika Shindano la Total Startupper of the year 2019 Mshindi ni  Doreen Noni ambaye amewapiku Vijana wengine 15 na kuzawadiwa kiasi cha Tsh 30,000,000.

Share To:

Post A Comment: