Mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Wanawake Tanzana Bara
maarufu kama Serengeti Lite Women’s Premier League unatarajiwa kuanza
kutimua vumbi siku ya Jumamosi, Machi 9 2019.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Soka la Wanawake, Amina Karuma amesema wanatarajia kuona
mzunguko wa pili unakuwa na ushindani kwa timu zote na hatimaye kupata
bingwa anayestahili.
Karuma
aliipongeza udhamini uliofanywa na Kinywaji cha Serengeti Premium Lite
ambao pamoja na mambo mengine umewezesha kuifanya ligi kuwa na ushindani
mkubwa na kuleta mvuto wa aina yake.
“Ligi
Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premier League imeweza kuleta ushindani
mkubwa baina ya timu zinazoshiriki na hata ukitazama matokeo unaweza
kuona ni jinsi gani ambavyo ligi hii imekuwa na msisimko wa aina yake,”
alisema
Aliongeza kuwa
katika kuhakikisha mzunguko wa pili unakuwa bora Zaidi, imefanyika
semina ya viongozi wa klabu na Waamuzi Wanawake ili kuwajengea uwezo
zaidi.
Kwa upande wake,
Ofisa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) ambao ni wadhamini
wakuu wa Ligi hiyo, George Mango alisema kudhamini ligi hiyo kupitia
kinywaji chake cha Serengeti Lite kumelenga kuongeza hamasa na kuleta
ushindani wa ligi hiyo ya wanawake.
“Katika
mzunguko wa kwanza tumeshuhudia hamasa na ushindani mkubwa miongoni mwa
timu zinazoshiriki ligi hii hivyo ni matarajio yetu kwamba mzunguko huu
wa pili utakuwa bora zaidi kwa timu zote ili kuongeza zaidi ari ya
ushindani,” alisema.
Kampuni
ya bia ya Serengeti (SBL) kupitia kinywaji cha Serengeti Lite imeweza
kuwekeza jumla ya Sh450 Milioni kama ufadhili wa ligi hiyo ya wanawake
nchini kwa kipindi cha miaka mitatu kama sehemu ya kuendeleza michezo
hususan mpira wa miguu nchini.
Aidha,
SBL imekuwa ikitilia mkazzo uendelezaji wa michezo nchini hasa katika
mpira wa miguu ambao mbali na kupendwa na watu wengi umekuwa chachu
katika kuinua vipaji mbalimbali nchini.
TIMU ZA LIGI KUU YA WANAWAKE (SWPL)
1. KIGOMA SISTERZ- KIGOMA
2. SIMBA QUEENS – DSM
3. ALLIANCE GIRLS –MWANZA
4. BAOBAB QUEENS – DODOMA
5. MLANDIZI QUEENS – PWANI
6. JKT QUEENS – DSM
7. PANAMA – IRINGA
8. EVERGREEN –DSM
9. MARSH ACADEMY – MWANZA
10. MAPINDUZI QUEENS – NJOMBE
11. YANGA PRINCESS –DSM
12. TANZANITE – ARUSHA.
Cliford Mario Ndimbo
Afisa Habari na Mawasiliano,TFF
Machi 8,2019
Post A Comment: