WhatsApp%2BImage%2B2019-03-08%2Bat%2B4.33.59%2BPM
 Mwenyekiti wa UVCCM taifa Kheri James (aliyesimama, mstari wa mbele)akizungumza na viongozi wa UVCCM Mkoa wa Pwani mara baada ya kuwasili Mkoani hapo na kukagua mradi wa ujenzi wa Chama, Leo Kibaha Pwani.
WhatsApp%2BImage%2B2019-03-08%2Bat%2B4.34.33%2BPM
 Mwenyekiti wa UVCCM taifa Kheri James akiwasikiliza wakandarasi wa mradi huo ambao umekamilika kwa asilimia 50, na amewataka vijana kuchangamkia fursa hizo zinazotolewa kwa ajili yao kupitia umoja wao wa vijana (UVCCM) leo Kibaha, Pwani.
WhatsApp%2BImage%2B2019-03-08%2Bat%2B4.36.18%2BPM
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani Charangwa Makwillo (aliyesimama kushoto) akitoa maelezo ya mradi kwa Mwenyekiti wa UVCCM taifa Kheri James mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi wa chuo cha Chama Mkoani humo, Makwillo amekishukuru Chama cha Mapinduzi kupitia umoja wa vijana kwa kutoa ajira 400 kwa vijana Mkoani humo, Leo Mkoani Pwani.



MWENYEKITI wa UVCCM taifa Kheri James leo amefanya ziara na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi chuo cha chama kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani. Mradi wa ujenzi wa chuo hicho uliwekwa jiwe la msingi na Rais Dkt. John Magufuli na hadi sasa umekamilika kwa asilimia 50 na hadi kufikia June 2020 mradi huo utakamilika.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo James amewataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ya awamu ya tano na kueleza kuwa hadi sasa zaidi ya vijana 400 wameajiriwa kupitia miradi hiyo huku Katibu mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally akitoa fursa kwa vijana kutoa mawazo yao kupitia umoja wao wa vijana.

Makamu Mwenyekiti UVCCM, Tabia Mwita amewataka vijana kujiandaa kwa fursa Zitakazotokana na chuo hicho na ametoa wito wa kuzingatia  usawa wa jinsia kwa kuhusisha na siku ya leo ya wanawake duniani. Kwa upande wake katibu mkuu UVCCM Mwalimu Mangwala amesema kuwa mradi huo umewalenga vijana na mafunzo yatakayotolewa ni kwa ajili ya kuwaandaa vijana katika kufahamu historia, itikadi na mwelekeo wa Chama.

Pia Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani Charangwa Makwillo ameushukuru uongozi wa UVCCM na serikali kwa ujumla kwa kutoa ajira zaidi ya 400 kwa vijana Mkoani humo. Imeelezwa kuwa Chuo hicho kitajenga wazalendo na viongozi wengi kutoka vyama dada vya MPLA, ANC,SWAPO na FRELIMO.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: