Wingu la simanzi limetanda katika kijiji cha Sisokhe eneo bunge la Likuyani kaunti ya Kakamega nchini Kenya  baada ya mwalimu mkuu aliyekuwa ameenda kwa mganga wa jadi kufariki dunia katika mazingira tatanishi.

Vivian Atuvuka aliaga dunia Jumatatu Machi 11,2019 muda mfupi baada ya kufika nyumbani kwa mganga huyo ambaye anadaiwa kumtenga kwenye chumba kimoja kando na wateja wengine. 

Inaelezwa kuwa Vivian Atuvuka anasemekana kugombana na jirani yake kuhusu mpaka wa shamba hivyo basi, alifika kwa Mganga huyo wa jadi kwa ajili ya kupata msaada kutoka kwa mganga jinsi angekabiliana na jirani huyo.

Inaarifiwa kuwa mganga Beatrice Okumu alimkuta Atuvuka akiwa ameshafariki dunia wakati wake wa kumhudumia ulipowadia.

 Mwalimu huyo alitaka ushauri kutoka kwa mganga jinsi angekabiliana na jirani wake kuhusu mzozo wa mpaka wa shamba.

"Alilalamika kuhusu maumivu ya kichwa na akanywa pakiti ya maziwa aliyokuwa nayo kwenye mkoba wake akisubiri kuhudumiwa,"Dismas Okum ambaye ni mumewe mganga huyo alisema.

 Mhudumu wa boda boda aliyempeleka Atuvuka kwa mganga huyo alisema alikuwa mchangamfu sana na hakuonyesha dalili zozote za kuwa mgonjwa.

Kulingana na mhudumu huyo wa boda boda, mwalimu huyo amekuwa akizozana na jirani wake kuhusu mpaka wa shamba kwa muda mrefu. 

Mmoja wa jamaa zake naye alisema mwalimu huyo hakuwa anaugua sana alipotoka nyumbani ila alikuwa amelalama kuhusu maumivu kwenye mkono wake wa kulia. 

Maafisa wa polisi wamemkamata mganga huyo ili aweze kusaidia katika uchunguzi kuhusiana na kifo cha mwalimu huyo. 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: