Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Rais wa
Chama cha Riadha Tanzania, Anthony Mataka (wa pili kushoto) akimpongeza
mshindi wa kwanza katika mbio za kilomita 21 maarufu kamaTigo Kili Half
Marathon Emmanuel Giniki baada ya kuibuka mshindi. Wa kwanza kulia
aliyeshikilia mfano wa hundi kwa ajili ya kumkabidhi mshindi huyo ni ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Kamuni ya Tigo Simon Karikari
Baadhi ya Wafanyakazi wa Tigo
wakiwa na nyuso za furaha huku wakionyesha medali zao baada ya ‘kufuta
vilimia’ na kufanikiwa kumaliza mbio za kilomita 21 maarufu kama Tigo
Kili Half Marathon zilizofanyika mjini Moshi ambazo ziliwashirikisha
wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 50 duniani
Mshindi wa mbio za Kilomita 21
maarufu kama Tigo Kili Half Marathon Emmanuel Giniki akihojiwa baada ya
kufanikiwa kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio hizo zilizofanyika
mjini Moshi na kuwashirikisha wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 50 duniani
Mkurugenzi Mtendaji Tigo Simon
Karikari (wa kwanza kulia)akiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na
Michezo Dk. Harrison Mwakyembe pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Rais
wa RT Anthony Mtaka waki mkabadhili mfano wa hundi ya Sh milioni 1,
025,000 Falluna Abdi aliyeshika nafasi ya pili kwa wanawake kwenye mbio
za Kilometa 21 maarufu kama Tigo Kili Half Maratahon zilizofanyika mjini
Moshi.
……………………………
Na Mwandishi Wetu
MTANZANIA Emmanuel Giniki ameibuka
mshindi wa mbio za kilomita 21 maarufu kama Tigo Kili Half Marathon
zilizofanyika mjini MoshI.
Giniki amevunja mwiko kwa mbio
hizo ambazo kwa miaka mingi zimekuwa zikitawaliwa na raia wa kigeni na
husasani Wakenya ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiibuka washindi.
Akizungumza muda mfupi baada
ya kukabidhiwa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni mbili, Giniki
alisema anayofuraha kushinda mbio hizo na kuiletea heshima nchi yake
jambo ambalo amekuwa akilitamani.
“Pamoja na kwamba mbio hizi
zimekuwa zikifanyika hapa nyumbani, tumekuwa tukishindwa kuzitendea haki
kwa kuwa wageni ndiyo wamekuwa wakizitawala. Ninayofuraha leo nimeweza
kulitoa taifa langu kimasomaso,” alisema.
Akiongea wakati wa halfa ya
kukabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Simon Karikari alisema
kampuni yake inayofuraha kuchangia maendelea ya michezo nchini na
hususani riadha ambayo pia huboresha afya
Karikari alisema Tigo imekuwa
mdhamini wa mbio za Kili half Marathon kwa kipindi ch miaka minne
mfululizo na kuongeza kuwa itaendelea kudhamini pamoja na kuboresha mbio
hizo kila mwaka.
Waziri wa Habari, utamaduni
vijana na Michezo Dk Harrison Mwakyemba aliishukuru Tigo kwa kudhamini
mbio hizo na kuwataka wakazi wa Moshi kutumia fursa zitokanazo na mbio
hizo kujijenga kiuchumi.
“Mbio hizi zimeleta wakimbiaji
kutoka nchi zaidi ya 50 hapa mjini Moshi. Idadi hii kubwa ya watu
itokanayo na mbio hizi ni fursa nzuri ya kibiashara na ni vyema wakazi
wa Moshi wakaichangamkia,” alisema Waziri Mwakyembe.
Mbio za Kilimanjaro Marathon
hufanyika mjini Moshi kila mwaka. Idadi ya washiriki wa mbio hizo
imekuwa ikiongezeka kwa mujibu wa waandaaji kutoka wakimbiaji 750 wakati
za kikianza hadi kufikia washiriki 11,000 kwa sasa.
Post A Comment: