Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa ndani ya gari lililobeba mabomba yanayoelekea kwenye jimbo lake kwa ajili ya mradi wa maji wa Mlandizi Mboga baada ya kutembelea kiwanda cha Mabomba cha Tanzania Steel Pipes leo Jijini Dar es Salaam.
Gari iloyobeba mabomba kwa ajili ha ujenzi wa mradi wa maji wa Mlandizi Mboga likiwa tayari kwa ajili ya safari ya kuelekea Chalinze.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Mhandisi Arone Joseph akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa ziara ya Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete (kushoto) kwenye kiwanda cha Mabomba cha Tanzania Steel Pipes leo Jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa anakagua eneo lilalotengenezwa mabomba ya kusambazia maji yatakayotumika kwenye mradi wa maji Mlandizi Mboga leo Jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa anakagua eneo lilalotengenezwa mabomba ya kusambazia maji yatakayotumika kwenye mradi wa maji Mlandizi Mboga leo Jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Chalinze akielezea kwa umakini ramani ya mradi wa Mlandizi Mboga unaotarajiwa kuanza kujengwa Katikati ya mwezi April mwaka huu utakaohudumia wakazi wa jimboni kwake akiwa sambamba na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Mhandisi Arone Joseph na Mkurugenzi wa Miradi DAWASA Mhandisi Lydia Ndibalema.
MBUNGE wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ametembelea kiwanda cha mabomba cha Tanzania Steel Pipes kinachotengeneza mabomba ya kusafirishia maji kwenye mradi wa maji wa Mlandizi- Chalinze- Mboga.
Akitembelea kiwanda hicho, Ridhiwani amefurahishwa na maendeleo ya utengenezaji wa mabomba hayo ambapo takribani mabomba 321 yameanza kusafirishwa kwa ajili ujenzi wa meadi huo unaotarajiwa kuanza katikati ya mwezi April.
Akizungumza baada ya kumaliza kukagua mabomba hayo, Ridhiwani amesema kuwa imechukua miaka 16 kwa wananchi wa Chalinze kupata majisafi na salama na imani yake kubwa ipo kwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA wafanikishe mradi huo.
Amesema, kukamilika kwa mradi huo ambao wameahidi utakuwa umekamilika katika kipindi cha miezi mitano hadi sita utaweza kulinda kiti chake cha Ubungo kwani wananchi wamekuwa wanamsumbua kwa kipindi kirefu.
“Sikuwahi kuona namna wananchi wanatumia maji pamoja na wanyama kama ng’ombe ila kukamilika kwa mradi huu kutawezesha watu wangu kupata majisafi na salama ila na wao kwa upande wao nitawaomba walipie huduma ili kuweza kuendesha miradi hii maji yaweze kupatikana,”amesema Ridhiwani.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Arone Joseph amesema mradi huo utawanufaisha wakazi wa maeneo hayo ikiwa pamoja na wananchi wanaoishi kwenye eneo la mradi.
Joseph amesema Mradi wa maji wa Mlandizi -Mboga unatarajiwa kusafirisha maji lita milioni 9.3 (mita za ujazo 9300) kwa siku kiasi kianchokisiwa kuweza kutosheleza mahitaji ya walengwa kwa sasa na ongezeko la matumizi kwa siku za usoni.
“Hadi sasa, kiasi cha mabomba ya umbali wa km 3.7 yameshazalishwa katika kiwanda cha TSP na yameanza kupelekwa kwenye maeneo ya mradi ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza katika Vijiji vya Mboga na Msoga,” amesema Joseph.
“Katika usanifu wa mradi huo, umetilia maanani ongezeko la watu na mahitaji ya miaka 20 ijayo na kutosheleza idadi ya watu hadi kufikia 120,912 ndani ya eneo la mradi na utakuwa kwa umbali wa Kilomita 58 ujenzi wa vituo viwili vya kusukumia maji na utagharimu bilion 14 hadi kukamilika kwake,”amesema Joseph.
Afisa Utawala wa Kiwanda cha Mabomba cha TSP, Elly Bohela amesema anashukuru sana kwa Mbunge Ridhiwani Kikwete kufika kwenye Kiwanda chao kuona namna wanavyotengeneza mabomba hayo ambayo yanaenda kuwekwa kwenye mradi uliopo katika jimbo lake.
Amesema, kiwanda cha TSP ni cha wazawa na wamejizatiti kwenye kutengeneza mabomba yenye ubora aidha ameishukuru dawasa kwa kuweza kuwaamini na kuwapatia kazi hiyo muhimu.
Maeneo yatakayohudumiwa na mradi huo ni pamoja na Ruvu darajani, Vigwaza,Ranchi ya Taifa Ruvu (NARCO), Chahua -Lukenge, Visenzi, Buyuni na Mdaula -Unebazomozi.
Kwingine ni Chamakweza, Pingi, Pera, Chalinze, Chalinze Mzee, Msoga na Mboga aidha, viwanda vitakavyofaidika ni pamoja na Twyford, kiwanda cha ngozi, kiwanda cha Matunda cha Sayona pamoja na watumiaji wengine wakubwa ikiwemo kampuni Yapi Merkezi wajenzireli ya kisasa (SGR).
Post A Comment: