Mhe Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Maji, Mahmoud Mgimwa(Aliyesimama) akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina na Mjumbe wa Kamati hiyo Calist Komu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina wa
pili kutoka kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali
waliohudhuria kikao hicho mara baada ya kumalizika
NA JOHN MAPEPELE,MWANZA
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametoa muda usiozidi mwezi mmoja kwa watendaji
wa Wizara yake kufanya marekebisho ya Kanuni Uvuvi ya Mwaka 2009 ili kuruhusu
kuvuliwa kwa samaki aina ya Sangara kuanzia sentimita 50 na kuendelea ili
kudhibiti utoroshwaji wa samaki hao kwenda nchi jirani na kuifanya Serikali na wadau
wa uvuvi kupata mapato makubwa zaidi kutokana na uhifadhi unaofanywa katika Ziwa Victoria.
Akizungumza
kwa katika kikao cha pamoja baina ya Kamati ya Bunge ya kudumu ya kilimo mifugo na maji na makundi ya wadau wa sekta uvuvi katika
ukumbi wa mkutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza mwishoni mwa wiki,Mpina
amesema kanuni ya sasa ya uvuvi inaruhusu kuvuliwa kwa Samaki Sangara kuanzia
sentimeta 50 hadi 85 hali ambayo inawafanya samaki wakubwa zaidi ya sentimita
85 kuuzwa katika nchi jirani kwa kuwa nchi nyingine zinaruhusu kuvuliwa kwa
samaki hao na Tanzania kubakia kuwa eneo la mazalia na malisho ya samaki hao.
“Wizara yangu haitalala itahakikisha
kwamba wananchi wananufaika na biashara ya samaki na mazao yake, lishe bora na
ajira zaidi zinazotokana na uhifadhi, sisi akina Mpina ni vibarua tu wa kulinda
raslimali za uvuvi kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye kwa hiyo tuendelee
kudhibiti uvuvi haramu ili uvuvi ututajirishe” alisisitiza Mpina
Aidha
ametoa muda wa wiki mbili kwa Taasisi ya Utafiti wa Samaki nchini(TAFIRI)
kushirikiana na wavuvi wa Bahari ya
Hindi kufanya utafiti wa vyavu za kuvulia dagaa mchele ili kupata majibu ya
kisayansi yatakayosaidia kutoa uamuzi wa kutumia nyavu za kutoka sentimeta 10 hadi sentimeta 8.
Waziri
Mpina alisema kutokana na udhibiti wa
uvuvi haramu uliofanywa na wizara yake
katika kipindi cha mwaka mmoja sasa ripoti iliyowasilishwa katika kikao cha Mawaziri
wa sekta uvuvi kwa nchi wanachama wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki wanazunguka ziwa Victoria jijini Arusha mwanzoni mwa mwezi
Machi mwaka huu inaonyesha kuwa samaki wazazi aina ya Sangara wameongezeka
katika ziwa Victoria kutoa asilimia o.4 ya awali hadi kufika asilimia 5.2
ambapo kwa kawaida inatakiwa
kufikia kiwango cha alisimia 3.3 huku
samaki waliokuwa wanaruhusiwa kuvuliwa (ambao ni sentimita 50-85) kuongezeka kutoka asilimia 3 hadi 32
na samaki wachanga kupungua kutoka asilimia 96.6 hadi 63.
Alisisitiza kuwa Serikali itaendelea
kusimamia kikamilifu Sheria ya Uvuvi Namba 22 ya Mwaka 2003 pamoja na Kanuni
zake za Mwaka 2009 ambapo aliongeza kuwa njia pekee kwa wavuvi ni kuzingatia
sheria badala ya kutaka kuonewa huruma
na vyombo vya Serikali huku wakiendelea kufanya uvuvi haramu.
Katika hatua nyingine Mpina ametoa
onyo kali kwa wamiliki wa viwanda vya kuchakata samaki kuacha mara moja kupuuza
maagizo ya Serikali ya kuwataka kuzingatia bei elekezi ya kuanzia shilingi 5500
kwa samaki aina ya Sangara kutoka kwa wavuvi ambapo amesisitiza kuwa hatua za
kisheria zitachukuliwa kwa yoyote atakayebainika.
Alisema ni kosa kwa wamiliki wa viwanda
vya samaki kupunguza bei za kununua
Sangara kwa wavuvi kwa visingizio kuwa
bei imeshuka katika masoko ya kimataifa bila kutoa uthibitisho wowote.
Akitolea
ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizowasilishwa kwa Serikali na wadau wa
uvuvi Mpina alisema Wizara yake inatambua kumekuwa na changamoto na mapungufu katika sekta ya uvuvi nchini
ndiyo maana Wizara imeamua kuifumua
Sheria ya Uvuvi ili ifanyiwe marekebisho na kutunga Sheria nyingine ya utunzaji
wa viumbe kwenye maji ili wadau wote waweze kuchangia mawazo yao
na kuboresha ili iendane na mazingira ya sasa.
Pia
Mpina alisema Serikali imeamua kuruhusu
taa za mwanga wa jua na majenereta kwa wavuvi ambapo amesisitiza kuwa serikali
inaendelea na utafiti ili kuona teknolojia
Kuhusu
suala la kusafirisha samaki kwa kutumia gari
maalum na serikali
kutoruhusu kuchukua samaki kilo 20 hadi zilipiwe alisema kwamba
tayari Serikali ilishalitolea ufafanuzi kwamba
wananchi hawazuiliwi kubeba kiasi hicho cha samaki pia gari yoyote
inayozingatia usafi inaruhusiwa kubeba samaki.
Alionya
watanzania kuendelea kutumika kama madalali wa wafanyabiashara wa dagaa kutoka
nchi jirani na kujifanya kuwa ndiyo wanunuzi ilhali wanafanya hivyo
kukweka kulipa kodi za Serikali.
Akichangia
katika mkutano huo mbunge Mheshimiwa Emanuel Papiani alipongeza juhudi
zinazofanywa na Wizara ambapo aliwataka wamiliki wa viwanda vya kuchakata
samaki kufanya biashara kwa uaminifu na
kufanya biashara zao kwa uwazi na
kushirikiana na serikali tofauti na ilivyo sasa ambapo wamekuwa wanashusha bei
za samaki bila kuishirikisha Serikali na wadau wengine wa sekta ya hiyo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo,
Mifugo na Maji, Mahmoud Mgimwa aliipongeza Wizara kwa jitihada na mikakati mbalimbali inayoibuni kwa wavuvi
ili kuwasaidia waweze kupata manufaa na
shughuli za uvuvi
Mgimwa
alisema katika kipindi cha muda mfupi
Wizara imeanzisha Dawati maalum linaloshughulikia sekta
binafsi katika kuwaunganisha na fursa mbalimbali ambapo pia Wizara
imesaidia kuwashawishi benki ya kilimo
kuanzisha benki hiyo katika jiji la
mwanza ili kutoa mikopo kwa wavuvi.
Alisema
kamati yake imekuwa ikifanya kazi kwa
karibu na Wizara na
itaendelea kuisimamia na kutoa maelekezo
mbalimbali kwa niaba ya wananchi ili kuweka daraja baina ya serikali na
wananchi.
Alisema
alifarijika kuona kuwa maelekezo yote yanayotolewa na Kamati yake kwa Wizara
yanafanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na marekebisho ya Sheria ya Uvuvi na 22 ya
Mwaka 2003 ambapo aliwahakikishia wa wavuvi kuwa maoni yao yatazingatiwa katika
sheria mpya na kwamba wana fursa
mbili za kushiriki katika utoaji wa maoni hayo
yakifikishwa bungeni na kabla ya kufika bungeni.
Naye
mvuvi na mfanyabiashara wa mabondo onesmo Nzagamba amepongeza
juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano za kuwasilikiliza wadau
wa sekta ya uvuvi ambapo amesema maamuzi
na maelekezo ya Waziri Mpina yatawanufaisha siyo tu wavuvi bali wananchi wengi
masikini.
“Tunamshukuru Mheshimiwa Rais John Pombe Joseph
Magufuli na Serikali yake kwa kuendelea kutujali sisi wanyonge” alisisitiza
Nzagamba
Post A Comment: