Wananchi wa Kilwa Kivinje wakishangilia na kusalimiana
na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina
(Mb), mwenye koti la bluu mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa
hadhara. Picha na John Mapepele
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa
Luhaga Joelson Mpina (Mb), mwenye miwani akiwasili katika eneo la
Kilwa Kivinje kuongea na wavuvi hivi karibuni. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa
Christopher Emil Ngubiagai na kushoto ni diwani Ali Mohamed Yusufu.Picha na John
Mapepele
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina
(Mb) akiwahutubia wananchi wa Somanga Kilwa. Picha na John Mapepele
|
Na
John Mapepele, Kilwa
Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Luhaga Mpina ametangaza kuundwa kanda kuu mpya ya ulinzi wa rasilimali
katika Bahari ya Hindi ili kukabiliana na uvuvi haramu ulioshamiri kwa
muda mrefu.
Amesema kuwa Serikali
ya awamu ya tano ina nia thabiti ya kulinda rasilimali hizo ili ziweze
kulinufaisha Taifa.
Mpina alitangaza uamuzi
huo hivi karibuni wakati akizungumza na wavuvi wilayani Kilwa mkoani
Lindi kuhusiana na juhudi zinazofanywa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi
katika kulinda rasilimali hizo na kutolea ufafanuzi wa baadhi ya maombi
ya wavuvi ikiwemo kuomba kuruhusiwa kutumia majenereta na taa za sola
kaatika shughuli zao za uvuvi wawapo baharini baada ya Sheria ya Uvuvi
ya mwaka 2003 kukataza za vifaa hivyo.
Akizungumza kwa nyakati
tofauti na wavuvi katika maeneo ya Kivinje na Somanga wilayani Kilwa
Waziri Mpina alisema Serikali ya awamu ya tano haina nia kumuonea mwananchi
yeyote bali kinachofanyika ni kulinda rasilimalli hizo kwa mujibu wa
sheria ili ziwe enedelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Mpina alisema katika
kuwasikiliza wavuvi nchini Serikali imeamua kufumua Sheria ya Uvuvi
na kanuni zake za mwaka 2009 ili kuondoa maeneo ambayo yanakwaza shughuli
za uvuvi ikiwemo kufuta vipengele vilivyokuwa vinalalamikiwa kwa muda
mrefu.
Hata hivyo Mpina alikubali
ombi la wavuvi nchini kurusiwa kutumia taa za sola na majenereta huku
akitaka wavuvi ha kutokamatwa kwa makosa ya kutokuwa na leseni hadi
hapo kanuni mpya zitakapotoa Julai mwaka huu.
Pia aliwaomba wavuvi
kuwa na subira kuhusiana na ombi la kutaka kuruhusiwa kutumia nyavu
za chini ya milimita nane kwani kwani sheria iliyopo ya uvuvi ya
mwaka 2003 na Kanuni yake ya mwaka wa 2009 imeweka masharti kuzuia matumizi
ya nyavu hizo kwenye ukanda wa bahari hivyo kuwataka kuwa watulivu na
kusubiri sheria hiyo ifanyiwe marekebisho.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa
christopher Ngubiagai alimshukuru Waziri Mpina kwa kufika kuzungumza
na wananchi hao kwani ametoa ufafanuzi utakaoondoa sintofahamu iliyokuwa
imetanda miongoni mwa wavuvi wa wilaya hiyo huku akiwaomba kuunga mkono
juhudi za serikali za kulinda rasilimali za uvuvi.
Mmoja wa wavuvi
wa Somanga Mohamedi Kimbwembe aliomba radhi Serikali ya awamu tano kutokana
na wavuvi wengi kujihusisha na uvuvi haramu na kuua mazalia ya samaki
na kwamba wengi walifanya hivyo baada ya serikali zilizopita kushindwa
kuchukuwa hatua dhidi ya waalifu hao.
Mbunge wa viti maalumu
mkoa wa Lindi Hamida Abdalha alimshukuru Waziri Mpina kwa kuruhusu matumizi
ya jenereta na taa za mwanga wa jua pamoja na kuruhusu wavuvi
kutumia leseni moja mambo ambayo yalikuwa yakiwaumiza wavuvi wa Lindi.
Post A Comment: