Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh.
Daniel Chongolo mkoani Dar es salaam akizungumza na waandishi wa habari
leo kwenye kituo cha Polisi cha Mbweni baada ya kufanya doria na
kukamata magendo ya vitu mbalimbali vilivyokuwa vikivushwa kutoka
Zanzibar kuja Tanzania Bara.
Vitu vilivyokamatwa katika doria
hiyo ni Sukari ya viwandani mifuko 75, Madumu ya mafuta ya kula 25 na
Pikipiki 2, vitu hivyo vimekuwa vikivushwa na Boti na kupokelewa na
Ngombe waliopata mafunzo maalum ambao kila mmoja anao uwezo wa kuchukua
mifuko 20 ya sukari na madumu kadhaa ya mafuta ya kula kutoka baharini
ufukweni mpaka nchi kavu na kupeleka kwenye maghala wanayohifadhia
mizigo hiyo moja kwa moja kwa maelekezo wanayopewa na wamiliki wa
ng’ombe.
Watu waliokamatwa wakituhumiwa
kujihusisha na uvushaji wa magendo hayo ni Ally Haruna Mnyamzwezi mkazi
wa Mbweni jijini Dar es salaam , Chauka Jonas Mwendesha Bodaboda mkazi
wa Mbweni Jijini Dar es salaam , Hamis Juma Mnyamwezi Mkazi wa Mbweni
Jijini Dar es salaam na mwendesha Bodaboda na Hemedy Ally Mshirazi
Kondakta mkazi wa Mbweni jijini Dar es salaam.
Mh. Daniel Chongolo amesema kama
mwawakilishi wa Rais na watetezi wa watanzania akishirikiana na jeshi la
polisi hawatakubali watu wachache waangamize wananchi kwa kuingiza
bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu, Tutapambana nao kikamilifu
na tutahakikisha tunakomesha hii biashara haramu ya bidhaa zisizokuwa na
viwango na zisizolipiwa kodi kuingizwa nchini.
Amesema “Tutahakikisha tunavunja
hizi bandari bubu zote katika fukwe za bahari ya hindi hasa maeneo ya
kuanzia Kawe, Mbweni kwenda katika mpaka wa Bagaoyo na Dar es salaam
ili kukomesha biashara hii”, Sukari iliyokamatwa ni ile inayotumiaka
viwandani ambayo haifai kwa matumizi ya binadamu.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh.
Daniel Chongolo mkoani Dar es salaam akisisitiza jambo wakati akitangaza
kukamatwa kwa bidhaa za magendo ambazo pia hazina viwango kwa matumizi
ya binadamu, Sukari hiyo na mafuta ya kula vimekamatwa kwenye bandari
bubu za Mbweni jijini Dar es salaam.
Kama inavyoonekanamifuko ya
sukari ya viwandani na mafuta ya kula vikiwa katika kituo cha polisi
Mbweni Konondoni jijini Dar es salaam.
Mkuu wa upelelezi Wilaya ya
Kipolisi ya Kawe ASP Dk. Ezekiel Kyogo akiwaelezea waandishi wa habari
jinsi oparesheni hiyo ilivyoendeshwa na kuwanasa watu hao.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh.
Daniel Chongolo mkoani Dar es salaam na Mkuu wa upelelezi Wilaya ya
Kipolisi ya Kawe ASP Dk. Ezekiel Kyogo wakionesha vifaa hivyo mbele ya
waandishi wa habari.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh.
Daniel Chongolo mkoani Dar es salaam na Mkuu wa upelelezi Wilaya ya
Kipolisi ya Kawe ASP Dk. Ezekiel Kyogo wakiowaonyesha Ng’ombe
wanaotumika kufaulisha magendo hayo.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh.
Daniel Chongolo mkoani Dar es salaam na Mkuu wa upelelezi Wilaya ya
Kipolisi ya Kawe ASP Dk. Ezekiel Kyogo wakiowaonyesha Ng’ombe
wanaotumika kufaulisha magendo hayo.
Mmoja wa maaskari wa kituo cha
Polisi Kawe akionyesha jinsi ng’ombe hao walivyo na uwezo wa kubeba
mizigo na kasi kubwa watembeapo kutoka eneo la bandari bubu hizo na
kuelekea kwenye maghala yanayohifadhi magendo hayo.
Post A Comment: