Mwandishi David Maphone.D'Salaam
12 March 2019.
Chama cha Wananchi (CUF) leo Tarehe 12/03/2019 kimepitisha kwa Kauli Mona Mabadiliko ya KATIBA kupitia Mkutano Mkuu unaoendelea kufanyika hivi sasa.
Katika Mabadiliko hayo Katibu Mkuu wa Chama kuanzia Leo atakuwa Katibu wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa kwa Mwenyekiti KUPENDEKEZA majina. Mawili na kuyapeleka kwenye BARAZA KUU LA UONGOZI kwajili ya kupigiwa Kura na kupatikana JINA MOJA LA KATIBU MKUU.
Mara baada ya kupitishwa kwa Mabadiliko ya Katiba kwa vipengere mbalimbali ikiwemo kuanzishwa kwa nafasi ya Makamo mwenyekiti kwa Upande wa Tanzania Bara, hivyo kuwapo kwa makamo wawili wa Mwenyekiti Tanzanian Bara na Tanzania Zanzibar.
Wajumbe wa MKUTANO MKUU wapatao (1,200) kama sijakosea walilipuka Kwa SHANGWE iliyojaa Matumaina kana kwamba wamekikomboa Chama kutoka kwenye MIGOGORO ya kipuuzi.
Baada ya kumalizika AGENDA ya kwanza Wajumbe wakijianda kupata Mapumziko ili kuingia kwenye Agenda nyingine, ndipo Jeshi la POLISI walifika na kuhitaji MKUTANO MKUU usiendelee kwa hoja kwamba wameambia na Joram BASHANGE kwamba Umezuiliwa na Mahakama.
Walipoulizwa na Viongozi wa CUF waonyeshe Zuio la Mshakama la MKUTANO MKUU walisema hawana labda wamipigie BASHANGE ndio mwenye Zuio hilo. Baada ya mawasiliano na BASHANGE Jeshi la POLISI walipatiwa na mteja wao BASHANGE hukumu ya Tarehe 08/03/2019 la kesi Mamba 248/2018 inayozuia watu LIPUMBA, SAKAYA, NGOLE na wengine Kuitisha MKUTANO MKUU.
Ndipo walipopewa Elimu kwamba MKUTANO MKUU huo haukuitishwa na LIPUMBA wala SAKAYA Umeitishwa na BARAZA KUU LA UONGOZI kwa mujibu wa Mamlaka yaliyotokana na KATIBA ya CUF ya mwaka 1992 Toleo la 2014 Ibara 77(2) na wakati hukumu hiyo inatoka BARAZA KUU LA UONGOZI lilikwisha Itisha MKUTANO MKUU na hakuna Zuio lolote kwa Chombo hicho kutoitisha MKUTANO MKUU na hakuna Zuio lolote la Mahakama kuhusu kufanyika kwa MKUTANO MKUU huo. na kama lipo basi walitoe.
JESHI LA POLISI wamejirithisha pasinashaka yoyote kwamba hakuna Zuio la MKUTANO MKUU ila kuna Zuio la watu TENA kwa majina yao wasiitisha MKUTANO MKUU, Hivyo Jeshi la POLISI wakasema endeleeni na MKUTANO WENU MKUU na sisi tunaimalisha Ulinzi.
.
MAONI YANGU.
.
Kwa kuwa MKUTANO MKUU umepitisha Mabadiliko ya KATIBA kwa Kauli Moja na nafasi ya KATIBU MKUU wa Chama sasa itakuwa ni Katibu mkuu wa KUTEULIA badala ya Kuchaguliwa Kuanzia Leo Tarehe 12/03/2019 MAALIM Self Sio TENA KATIBU MKUU wa CUF.
Kurejea kwenye nafasi yake kutategemea Mwenyekiti wa chama Taifa atakaye chaguliwa kama akimpendekeza kati ya majina mawili ili kupigiwa kura na Wajumbe wa BARAZA KUU LA UONGOZI.
Niwapongeze Wajumbe wa MKUTANO MKUU kwa kufanya Mabadiliko ya KATIBA itakayosaidia kuondoa MIGOGORO ndani ya Chama. PROPAGANDA zinazo fanywa Mitandaoni kwamba MKUTANO MKUU umezuiliwa niza kupuuza na hazina nafas kabisa, MKUTANO MKUU unaendelea na sasa ni uchaguzi wa Viongozi mbalimbali kwa mujibu wa KATIBA ya CUF.
.
USIONDOKE HAPA KWA HABARI SAHIHI ZA MKUTANO HUU.
.
Mwandishi David Maphone
0714304970
DSM.
Post A Comment: