Mkurugenzi wa Kampuni Otterlo Bussiness Cooperation (OBC) Isaya Mollel akiwasili katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ambapo alisomewa mashtaka kumi 10.Picha na Ferdinand
Shayo.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ambapo alisomewa mashtaka kumi 10.Picha na Ferdinand
Shayo.
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Mkurugenzi
wa Kampuni Otterlo Bussiness Cooperation (OBC) Isaya Mollel amesomewa mashtaka 10 ikiwemo uhujumu uchumi ,utakatishaji wa fedha kifungu
cha 12 (c) cha sheria ya utakatishaji wa fedha haramu namba 12 ya mwaka
2006,pamoja na kukwepa kodi kiasi cha shilingi bilioni 2.8 pamoja na kosa la kughushi nyaraka .
Mollel
amefikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kusomewa mashtaka 10 na
Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) Oswarld Tibabyekomya ambapo mtuhumiwa
amewakilishwa na Joho la mawakili wakiongozwa na Wakili Method Kimomogolo.
Aidha Hakimu
Mfawidhi wa Mahakama hiyo Niku Mwakatobe amesema kuwa Mahakama hiyo haina uwezo
wa kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi hivyo kesi hiyo itatajwa tena March 18
mwaka huu.
Kaimu Mkuu
wa Takukuru mkoa wa Arusha Frida Wikesi
amesema kuwa wamemshikilia mkurugenzi huyo wa OBC alishikiliwa na Takukuru na
kuhojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani ambapo amesomewa mashtaka yanayomkabili.
Frida ametoa
onyo kwa Viongozi wa serikali na taasisi kutojihusisha na vitendo vya rushwa
kwa ni hawatasita kuwachukulia hatua.
Post A Comment: