Mkurugenzi wa Manispaa Ilala Jumanne Shauri |
Na Heri Shaaban
MANISPAA ya Ilala Dar es Salaam imesema kwamba inatarajia kumuamisha shule ya sekondari Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo kata ya Msimbazi, kufuatia kulalamikiwa katika kikao cha Baraza la madiwani Mkuu wa Shule hiyo kushindwa kusimamia nidhamu kwa Wanafunzi.
Sakata la shule ya sekondari hiyo liliibuka katika kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala na Diwani wa Viti Maalum Saada Mandangwa wakati alipokuwa akichangia hoja yake iliyoibua mshtuko katika kikao hicho.
Akiwasilisha hoja hiyo Diwani wa Viti maalum (CCM) Saada Mandangwa alisema kwa sasa hali ni mbaya katika shule hiyo kufuatia Wanafunzi wa shule hiyo ya sekondari kudaiwa, kukosa nidhamu hali inayopelekea wanafunzi kufanya vibaya kitaaluma.
"Tunakuomba Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala uondoe uongozi wote wa shule mkuu wa Shule hiyo ameshindwa kuthibiti wanafunzi wanaichafua shule "alisema Saada
Alisema shule hiyo kwa sasa imeharibika hivyo ofisi ya Mkurugenzi ingilia kati uchukue hatua na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo asaidiwe huenda ameshindwa kukabiliana na hali hiyo.
Aidha pia Madiwani hao walimshauri Mkurugenzi wa Manispaa Ilala kujenga uzio wa shule kwa ajili ya kudhibiti wanafunzi kwani kukosekana kwa uzio ni sababu moja wapo inayochangia wanafunzi hao kujiingiza katika vitendo viovu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa Ilala Jumanne Shauri alikiri kuwepo kwa taarifa za shule hiyo na kwamba hatua kali zitachukuliwa kudhibiti hali hiyo.
"Shule kukosa uzio sio sababu ya Wanafunzi wa shule ya sekondari hiyo kufanya vibaya tutamuamisha Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,kisha tutawadhibiti wanafunzi Wanaojiusisha na matukio ya kiuni"alisema Shauri.
Shauri aliagiza shule zote za halmashauri hiyo kuwa na nidhamu shuleni kuzingatia masomo ili kufanya vizuri kitaaluma.
Wakati huohuo Mkurugenzi wa Manispaa ya Jumanne Shauri alisema katika Baraza hilo kuwa suala la kugawanywa Majimbo na Wilaya hiyo kwa sasa ana taarifa hizo za kugawanya mitaa, Majimbo wala Wilaya.
"Suala la kugawanywa Kata, Mitaa, majimbo na Wilaya mwenye Mamlaka Waziri mwenye dhamana bado halmashauri hatujaletewa maelekezo"alisema
Alitoa majibu hayo wakati wa kujibu swali la lililoulizwa na Diwani wa kata ya Msongola Azizi MWALILE akitakata kufahamu serikali ina mpango gani kuhusiana na ukubwa wa Kata zilizopo manispaa ya Ilala.
Naye Diwani wa kata ya Ilala Saddy Kimji amelalamikia Mkandarasi wa Usafi kata ya Ilala akitaka aondolewe amekosa sifa.
Pia malalamiko mengine ambayo ametoa katika Baraza hilo alisema fedha nyingi zimetumika katika ujenzi Wa Mtaro mkubwa wa Buguruni Malapa lakini matunzo yake madogo.
Mwisho
Post A Comment: