Washiriki wa warsha ya
utetezi wa sheria za vyombo vya habari iliyoandaliwa na kuendeshwa na MISA
kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la
ICNL.
Na Mwandishi
Wetu
Katika kuendeleza hamasa na
kutetea uhuru wa kujieleza katika jamii, MISA Tanzania na shirika la
utetezi wa sheria na haki za kijamii la ICNL zimewakutanisha wadau mbali
mbali katika warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari.Warsha hiyo
imehudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya habari,asasi za utetezi wa
haki za binadamu ,wanasheria pamoja na wahadhiri wa vyuo vikuu.
Warsha hiyo ya
siku mbili iliyofanyika mjini Bagamoyo ililenga kuwakutanisha wadau hao kwa
lengo la kuzifahamu,kuzielewa na kujadili namna sheria za vyombo vya habari
zinavyo athiri mazingira ya kazi za kiuandishi pamoja na uhuru wa kujieleza
kuanzia ngazi ya taifa hadi kimataifa.
Kaimu mkurugenzi wa MISA
Tanzania Gasirigwa Sengiyumva akikaribisha washiriki na kutoa neno la
ufunguzi katika warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya
habari.
Akizungumza wakati wa ufunguzi
Kaimu Mkurugenzi wa MISA Tanzania Gasirigwa Sengiyumva alitoa wito kwa
wadau wa masuala ya habari kuendelea kupaza sauti bila kuvunja sheria
akisisitiza uhuru wa kujieleza ni haki ya kila mmoja.
Kadhalika
akielezea umuhimu wa uwepo wa sheria rafiki katika kufanya mazingira yawe
salama kwa tasnia ya habari,Bw.Aloys Habimana kutoka shirika la kimataifa
la utetezi wa haki za kijamii la ICNL lenye makao makuu yake nchini
Marekani amesema changamoto ya sheria zisizo rafiki kwa taaluma ya habari
na uhuru wa kujieleza ni changamoto sehemu nyingi duniani Afrika ikiwa na
mifano halisi.
Bw.Aloys
Habimana kutoka shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL
akiendesha warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari iliyoandaliwa
na kuendeshwa na MISA kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la utetezi
wa haki za kijamii la ICNL.
"Pamoja na mazingira haya nawasihi
msivunjike moyo wala kukata tamaa, masuala ya kisheria hayabadiliki kwa
siku moja yanahitaji kupitia hatua kadhaa na kila jambo linaweza kupatiwa
ufumbuzi hasa wadau wote watakaposhirikiana na kujenga hoja zenye ushawishi
na tija kwa pande zote", alisisitiza
Bw.Aloys.
Sambamba na
hilo Bi.Lily Liu mjumbe kutoka ICNL aliahidi kuwa shirika lao litaendelea
kushirikiana na wadau husika katika nyanja zote ili kufanikisha na kutimiza
adhma ya kuwa na jamii isiyo na sheria kandamizi zinazoathiri dhana nzima
ya uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari.
Bi.Lily Liu kutoka shirika
la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL akijadili jambo pamoja
na wadau walioshiriki warsha hiyo.
Washiriki
warsha hiyo wakijadili baadhi ya sheria na kanuni katika
makundi.
Post A Comment: