Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Patricia
Fikirini,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa watumishi wa Mahakama,mafunzo yanayoendeshwa na Taasisi
ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Misa tan katika Hotel Ya Leopard mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Taasisi
ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (Misa Tan),Salome
Kitomary akizungumza wakati wa mafunzo kwa watumishi wa mahakama za mkoa wa Kilimanjaro.
Baadhi ya Watumishi wa mahakama wakishiriki mafunzo hayo yanayofanyika katika Hoteli ya Leopard mjini Moshi.
Mkurugenzi wa Misa Tan, Gasirugwa
Sengiyumva,akiwaleza washiriki wa mafunzo hayo shughuli mbalimbali ambazoo taasisi ya Misa Tan imekuwa ikifanya .
Washiriki
wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi ,Kaimu
Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Moshi ,Patricia Fikirini pamoja
na wakufunzi wakati wa ufunguzi rasimi wa mafunzo hayo .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya
Jamii,Kanda ya Kaskazini.
KAIMU Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Patricia
Fikirini,amesema kuwa mafunzo ya huduma kwa wateja na upatikanaji wa taarifa
kwa watumishi wa Mahakama ni muhimu kwa kuwa yatapunguza malalamiko kwa
watumiaji wa mahakama.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watumishi wa
mahakama za mkoa wa Kilimanjaro, Jaji Fikirini alisema mafunzo hayo yamekuja
kwa wakati muafaka kwa kuwa limekuwa ni hitaji la muda mrefu.
Mafunzo hayo yameendeshwa na Taasisi
ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Misa tan, kwa kushirikiana na Taasisi ya
Kijerumani ya Friedrich Ebert Stiftung, yanahusu huduma kwa wateja, upatikanaji
wa taarifa na maadili kwa utumishi wa umma.
“Mafunzo haya ni msingi wa
mabadiliko kwa kilio kwa wateja kutoridhishwa na huduma za mahakama.Natarajia
yatazingatiwa na kusaidia kuleta mabadiliko katika kuwahudumia wateja.”alisema
Jaji Fikirini.
Aidha, aliwataka watumishi hao
kuunda kukosi kazi cha ufuatiliaji wa utekelezaji wa mafunzo hayo ya jinsi
wanavyowahudumia wateja wanaofika mahakamani, ili kupunguza malalamiko ambayo
yanatoa taswira isiyo sahihi kwa mahakama.
Awali akimkaribisha Jaji Mfawidhi
Kanda ya Moshi, Patricia Fikirini, kufungua mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Taasisi
ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (Misa Tan),Salome
Kitomary alisema Misa Tan imepanga kutoa mafunzo mbalimbali kwa watumishi hao
wa mahakama.
Alisema mafunzo yatakayotolewa ni
pamoja na huduma kwa wateja, upatikanaji wa taarifa na maadili kwa watumishi wa
mahakama kwa Mahakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mahakimu wa Mahakama za
Wilaya, Mwanzo pamoja na watumishi wa mahakama na watunza kumbukubu 36 wa mkoa
wa Kilimanjaro.
Kitomary alisema washiriki hao
watafundishwa nini maana ya uhuru wa kujieleza (mambo muhimu na misingi yake),
huduma kwa wateja na ujuzi wa mawasiliano kwa watumishi wa umma.
Kadhalika, washiriki watajifunza
mifano ya utekelezaji wa uhuru wa kujieleza, Tanzania, Afrika na Duniani,
Matakwa ya kisheria ya uhuru wa upatikanaji wa taarifa, muundo wa vyombo/
taasisi za umma na upatikanaji wa taarifa.
Aidha, washiriki hao pia watajifunza
jinsi ya kutoa taarifa na kuomba taarifa, ujuzi wa misingi na sifa za
kushughulikia malalamiko ndani yake ikiwa ni muundo wa kushughulikia
malalamiko,manufaa ya kushughulikia malalamiko kwa wakati, kukabiliana na tabia
za ndani na jinsi ya kwuahudumia wateja wenye hulka tofauti na kukabiliana na
malalamiko kiufundi katika kukabiliana na hasira na majibu yenye mhemko.
Mada nyingine zinazotarajiwa
kuwasilishwa ni pamoja na kukabiliana na kazi zenye malalamiko ambayo ndani
yake ina kukubaliana na hatua inayofaa kwa wateja, kuwa wazi juu ya mamlaka/nguvu
ulizonazo, kuongezeka kwa malalamiko na mchakato wa usimamizi wa malalamiko,
kutoka maoni na kuheshimu ahadi.
Kwa siku ya tatu washiriki
watafundishwa au kukumbushwa juu ya kanuni za maadili na maadili kwa watumishi
wa umma, utaratibu wa mahakama katika kushughulikia malalamiko.
Mkurugenzi wa Misa Tan, Gasirugwa
Sengiyumva, alisema chanzo cha mafunzo haya ni mwaka 2004 baada ya
Mahakama kupata kufuli kwa kutofunguka kutoa taarifa kwa wananchi, utafiti huo
ulifanywa na Misa Tan, ukiangalia taasisi za umma ambazo zimefungaka zaidi na
ambazo hazikufunguka kutoa taarifa kwa wananchi wa kawaida kabisa.
Post A Comment: