Wadau wa sekta ya Utalii pamoja na wafanyabiasha kutoka maeneo mbalimbali Kanda ya kaskazini wamekutana jijini Arusha kwa lengo la kujadili changamoto za kibiashara na mifumo ya ulipaji fedha kwa njia ya mtandao.

Akizungumza na wadau hao mkuu wa kitengo Cha masoko kutoka Benki ya KCB  Christine Manyenye amesema ni wakati muafaka kwa taasisi za fedha kutumia Fursa ya ufanikishwaji wa malipo kwa njia ya mtandao (Online payment) ili kuweza kurahisha huduma kwa sekta ya Utalii nchini.


Suala ambalo litasaidia kwa asilimia kubwa Katika kumuwezesha mtalii wa ndani na nje kutimiza mahitaji yake wakati wa maandazi ya Safari za Utalii nchini.


Kwa upande wake msimamizi wa kitengo cha huduma kwa njia ya mitandao Priscus Kessy amesema kwa Sasa Benki hiyo tayari imeanza kutumia huduma ya malipo kwa njia ya mtandao nankusisitiza wafanya biashara kutumia Fursa hiyo ili kuendana nankasi ya serikali ya awamu ya tano Katika kuelekea nchi ya uchumi wa Kati wa Tanzania ya viwanda.


Amesema mifumo hiyo imekuwa ikirahisaha huduma za malipo kwa watalii kabla ya kuanza Safari wakiwa nchi mwao.


Nao baadhi ya washiriki wa Mkutano huo akiwemo Veronica na John Samuel wamesema awali imekuwa changamoto kwa watalii kukamisha suala la malipo kwa Kampuni zao lakini kuwepo kwa mfumo huo kutaongeza idadi ya watalii pamoja na changamoto kadhaa zianazo jitokeza katika sekta ya biashara ya Utalii.


Aidha,Msimamizi wa Maendeleo ya biashara kutoka kituo Cha Biashara Cha jumuiya ya Afrika mashariki (EABC) bi Angelika Farhan amesema kwa Sasa ushirikiano wa pamoja kwa nchi za jumuiya ya Afrika mashariki imekuwa Chachu ya Maendeleo kwa nchi hizo.


Ambapo ameweka wazi kwa asilimia kubwa vikwazo vya kibisha vimepunguzwa kwa maslahi mapana ya nchi EAC kibiashara.


Katika hatua nyingine Bi Angelika amesema ni wakati muafaka kwa taasisi za kifedha(Bank) kuongeza wigo ili kurahisha huduma za kibiashara kwa nchi za jumuiya ili kuchochoea Maendeleo.


Katika Mkutano huo zaidi ya washiriki 200 kutoka maeneo mbalimbali wamejitokeza kushiriki Mkutano huo ili kuweza kuchochea Maendeleo kwa sekta hiyo na  biashara kwa ujumla.



Share To:

msumbanews

Post A Comment: