Na Vero Ignatus, Arusha

MFUKO wa Fidia kwaWafanyakazi (WCF), umewataka  waajiri kuwa waadilifu juu ya uwasilishaji wa 
 taarifa zinazohusu idadi ya wafanyakazi wao na viwango vya mishahara wanavyowalipa.

Kauli hiyo imetolewa  na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo Dkt. Abdulsalaam Omary wakati wa semina ya mafunzo kwa mameneja waajiri kuhusu wajibu wa mwajiri katika kutekeleza sheria ya usalama na afya mahala pa kazi .

Amewataka waajiri kupeleka idadi sahihi ya wafanyakazi sambamba na  kuelimisha kuhusu kazi na shughuli za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) jijini Arusha.

“Niwaombe waajiri, mnapotuletea taarifa jaribuni kutuletea taarifa sahihi kuhusu idadi ya wafanyakazi mlio nao na viwango vya mishahara mnavyowalipa, kwani baadhi yenu huleta idadi pungufu ya wafanyakazi na wengine hamuwaorodheshi.” Alisema.

Kwa bahati mbaya wale ambao hamuwaorodheshi ndio wanaopatwa na matatizo ya ajali au maradhi yatokanayo na kazi na linapokuja swala la kudai fidia taarifa zao zinakuwa hazipo nahii sio sawa.” Alisema Dkt. Omary.

Alisema kuna waajiri ambao hawatoi mikataba kwa wafanyakazi kwa lengo la kukwepa wajibu.

“Kwa sheria ya WCF mfanyakazi asiye na mkataba na amehudumu katika kazi hiyo kwa siku 30 mfululizo, huyo anatambuliwa na Mfuko kama mfanyakazi anayetakiwa kusajiliwa na kulipiwa mchango wa kila mwezi.” Alifafanua.
 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omary,(kulia), akizungumza wakati wa semina ya kuwaelimisha mameneja waajiri kuhusu umuhimu wa kuzingatia sharia juu ya usalama na afya mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya vihatarishi vya ajali mara kwa mara ili kupunguza madhara yatokanayo na ajali kazini. Semina hiyo imefanyika leo Machi 28, 2019 jijini Arusha. Kushoto ni Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Naanjela Msangi
  Sehemu ya waajiri walioshiriki semina hiyo.
  Sehemu ya waajiri walioshiriki semina hiyo.
 Sehemu ya waajiri walioshiriki semina hiyo.
 Meneja Tathmini ya Usalama na Afya mahala pa Kazi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Naanjela Msangi, akitoa mada kuhusu umuhimu wa kufanya tathmini ya mara kwa mara mahala pa kazi.
 Afisa wa WCF, Bw. Edward Kirenga, Bw. Edward Kirenga, akitoa mada mbele ya washiriki.
 
 Mwakilishi wa ofisi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), jijini Arusha Bi. Zaria Mmanga (kulia), akizungumza mbele yawaajiri wakati wa semina ya mafunzo kuhusu masuala ya usalama na afya mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na shughuli za Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi WCF jijini Arusha Machi 28, 2019.
 Mwakilishi wa ofisi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), jijini Arusha Bi. Zaria Mmanga (kulia), akitambulishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge kwa waajiri wakati wa semina ya mafunzo iliyoandaliwa na WCF kuwaelimisha kuhusu wajibu wa waajiri na wafanyakazi katika kuhakikisha masuala ya usalama na afya mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na shughuli za Mfuko wa Fidia zinafahamika vema
 Picha ya pamoja ya washiriki.
Picha ya pamoja ya washiriki.
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: