Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Tandika, Geoffrey Isack Mwachisye pamoja na Diwani wa Kata ya Chikongola Musa Namtema (Fasheni) leo March 27, 2019, wametangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) wakitokea Chama cha Wananchi (CUF).
Wawili hao wamesema sababu kubwa ya wao kujiunga CCM ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa John Pombe Magufuli.
Post A Comment: