Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.
Mrisho Gambo akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti ofisini
kwake wakati Kamati hiyo ilipomtembelea kabla ya kuanza ziara yake
katika Mkoa huo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya
Bajeti wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.
Mrisho Gambo wakati Kamati hiyo ilipomtembelea ofisini kwake kabla ya
kuanza ziara yake katika Mkoa huo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya
Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. George Simbachawene wakiangalia
mitambo iliyotumika kutengeneza matairi katika kiwanda cha General Tyre
kilichoko Arusha, mwenye suti nyeusi ni Mkurugenzi wa Shirika la
Maendeleo (NDC), Profesa Damian Gabagambi. Wajumbe hao wapo katika ziara
ya siku saba Mkoani Arusha
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Bajeti , Mhe. George Simbachawene akizungumza katika kikao cha Kamati
hiyo na uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (AIA) wakati Kamati hiyo
ilipotembelea chuo hicho.kushoto kwake ni Naibu Mkuu wa Baraza la Chuo
hicho, Ndugu Juma Kaniki na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.
Mrisho Gambo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya
Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. George Simbachawene wakiwa katika
kikao cha pamoja na uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (AIA) wakati
Kamati hiyo ilipotembelea chuo hicho.
PICHA NA OFISI YA BUNGE
Post A Comment: