Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa ndani ya ndege ya Air Tanzania aina ya Airbus A220-300 wakati
akielekea nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa Africa Now Summit 2019
unaoanza kesho tarehe 12 mjini Kampala Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu
wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan amewasili nchini Uganda na kupokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya
Nje wa nchi hiyo Mhe. Philemon Mateke pamoja na Balozi wa Tanzania
nchini Uganda Dkt. Aziz P. Mlima katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Entebe.
Makamu wa Rais pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaru wamesafiri na ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la Tanzania aina ya Airbus A220-300 (Dodoma) kutoka jijini Dar es Salaam mpaka Entebe kupitia Kilimanjaro.
Makamu wa Rais pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaru wamesafiri na ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la Tanzania aina ya Airbus A220-300 (Dodoma) kutoka jijini Dar es Salaam mpaka Entebe kupitia Kilimanjaro.
Kesho
Makamu wa Rais atashiriki mkutano wa mwaka 2019 wa “Africa Now Summit
2019” ambao utafunguliwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni
ambapo viongozi mbalimbali wa Afrika wanakutana ili kupata majibu ya
changamoto za Afrika katika masuala ya kiuchumi.
Katika
mkutano huo wa Viongozi wa Afrika, Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambapo
katika mada mbalimbali zitakazojadiliwa Makamu wa Rais atazungumzia
suala la Uongozi unaohitajika kuchochea mabadiliko ya Kijamii na Uchumi
Afrika.
Viongozi
wengine watakaotoa mada ni Rais wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Umoja wa Afrika (UA) Mhe. Abdel Fattah el Sisi; Rais wa Afrika Kusini
Mhe. Cyril Ramaphosa; Makamu wa Rais wa Kenya Mhe. William Ruto; na
Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Ahmed Abiy na Rais Paul Kagame wa Rwanda.
Mada zote hizi zitajikita kwenye kuonesha chachu ya Uongozi katika
kuleta maendeleo endelevu barani Afrika.
Mkutano
utamalizika tarehe 13 Machi 2019 utaanza na hotuba kutoka kwa Rais wa
Somalia Mhe. Mohamed Abdullahi na baadae kufungwa rasmi na mwenyeji wake
Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.
Makamu wa Rais ataambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Dkt. Aziz
P. Mlima mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Entebe nchini Uganda. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Mhe.
Philemon Mateke mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Entebe tayari kwa kushiriki mkutano wa Africa Now Summit
2019 utakaofanyika mjini Kampala tarehe 12 na 13 mwezi Machi, 2019.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimsikiliza Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Dkt. Aziz P. Mlima (kulia)
mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebe,
wengine pichani ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa
Uganda Mhe. Philemon Mateke (kushoto).
Post A Comment: