Na Heri Shaaban
BARAZA la madiwani Manispaa ya Kinondoni wamewalalamika wafanyabiashara ndogondogo maarufu Wamachinga waliopewa vitamburisho vya Rais Magufuli kuwa chanzo cha uchafuzi wa Mazingira Manispaa hiyo.


Madiwani hao walitoa tamko hilo Dar es Salaam leo katika kikao cha Baraza la madiwani la halmashauri hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho Wilayani Kinondoni Diwani wa Mbezi Juu (CHADEMA) Fares Lupomo  alisema wafanyabiashara hao Wamachinga toka wapate vitamburisho vilivyotolewa na Rais Magufuli vya 20,000 wamekuwa wakifanya Biashara maeoneo sehemu zote ikiwemo barabarani na katika majumba ya watu bila kuzingatia usafi.

"Hali ya usafi katika manispaa ya Kinondoni sio nzuri kwa ujumla tunaomba kikao cha zarula madiwani, Wenyeviti wa serikali za mtaa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ili kuzungumzia changamoto hii katika manispaa yetu tunakuomba Katibu Tawala wa Wilaya na Meya ulibebe ili "alisema Lupomo.

Alisema Wamachinga toka wapewe ruhusa ya kufanya Biashara kwa kutumia vitamburisho hivyo Kinondoni imekuwa chafu na Dar es Salaam kwa ujumla.

Diwani Lupomo alisema Manispaa hiyo kwa sasa aina gari la kubeba takataka wamemuagiza meya kununua gari za takataka ili kunusuru hali hiyo kwa ajili ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko .

Kwa upande wake Meya wa Manispaa Kinondoni Benjamini Sita alisema wataweka utaratibu kwa ajili ya kuandaa kikao hicho  ,pia alisema halmashauri hiyo inaweza kununua gari 20 za kubeba takataka kazi ikafanywa na manispaa wenyewe au wakubaliane tenda wakawalipa kwa utaratibu.

Meya Sita alisema ikifikia wakati pia wameshindwa halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni itachukua jukumu la kubeba takataka wenyewe.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa KAMATI ya mipango miji na Mazingira Songoro Mnyonge alisoma taarifa ya robo ya Pili kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2018 idara ya mipango miji na ardhi katika kipindi cha robo ya pili imefanya kazi ya  utekelezaji shughuli mbalimbali ikiwemo kuandaa taarifa za kitaalam ya maombi 78 ya kubadili matumizi ya Ardhi na kuwasirisha katika vikao vya mipango miji.

Songoro pia alisema Jumla ya michoro 107 imefanyiwa marekebisho na kujadiliwa katika kikao cha Kamati ya mipango miji Oktoba na Desemba 2018.

Aidha alisema Jumla ya maombi 31 ya kugawanywa viwanja yamefanyika kazi na kuwasirishwa katika kikao cha Kamati ya mipango miji na Mazingira Oktoba na DESEMBA 2018,

"Idara yangu kitengo cha Ardhi Wameandaa hati 137 kwa njia ya kieletronick katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Kinondoni na kutoa vibali vya kuhamisha miliki 121vimetolewa 34 vimepokelewa "alisema Songoro

Share To:

msumbanews

Post A Comment: