Afisa Mtendaji wa Kata ya Segera wilayani Handeni Rukia Chizinga akizungumza wakati wa mdahalo wa elimu uliendeshwa kwenye shule ya Msingi Michungwani na Asasi ya Tree of Hope chini ya ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society.
Diwani wa Kata ya Segera (CCMI Akizungumza katika mdahalo huo
Mratibu wa Mradi wa Uhamasishaji na Uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka zinazohusika katika kuboresha huduma za elimu katika Halmashauri ya Handeni Goodluck Malilo akisisitiza jambo wakati wa mdahalo huo
Mwenzashaji Wakili Mazule akisisitiza jambo wakati wa mdahalo huo
Sehemu ya washiriki wa mdahalo huo wakifuatilia kwa umakini
Picha ya Pamoija |
MADEREVA
wa malori na madalali kata ya Segera wilayani Handeni mkoani Tanga ambao
watakutwa na watoto wakiwa wanapakia machungwa watakamatwa na kufunguliwa
mashtaka ya kuwafanyisha kazi ikiwemo kupelekwa mahakamani
Hayo yalisemwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Segera wilayani Handeni Rukia Chizinga wakati
wa mdahalo wa elimu uliendeshwa kwenye shule ya Msingi Michungwani na Asasi ya
Tree of Hope chini ya ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society.
Alisema kama
madalali na madareva wanakwenda kupakia machungwa lazima wahakikishe hawachukui
watoto chini ya miaka kumi na nane haijalishi anasoma au hasomi ili mradi wapo
chini ya umri huo watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
“Niwaambie
madereva wa malori na madalali kwamba yoyote tukaye mkuta na mtoto…Dereva
tutamfungulia mashtaka ya kumfanyisha mtoto kazi na kumpeleka mahakamani zamani
tulikuwa tunaishi Polisi wanalipa faini lakini pia wazazi walikuwa
wanachukuliwa hatua ila kwa sasa tutawafikisha mahakamani”Alisema Afisa
Mtendaji huyo
Aidha
alisema ili madereva hao na madalali waendelee kuwa salama wakati wa ufanyaji
shughuli zao wakati wa kupachia machungwa wahakikishe watoto walio chini ya
umri wa miaka kumi na nane hawahusiki kwenye kazi hizo.
Naye kwea
upande wake, Mratibu wa Mradi wa Uhamasishaji na Uwajibikaji wa Jamii na
Mamlaka zinazohusika katika kuboresha huduma za elimu katika Halmashauri ya Handeni
Goodluck Malilo alisema
katika awamu ya pili ya mradi huo wataangalia
namna ya ule wa awali ulivyoleta mabadiliko makubwa kwenye jamii husika ikiwemo
hali halisi ilivyo kwa sasa na kipindi kilichopita hususani kwenye mambo
waliokuwa wakiyaainisha kwenye midahalo yao.
“Wataangalia
suala la uwazi na uwajibikaji ikiwemo shule kuwa na ubao wa matangazo,tatizo la
utoro,changamoto za mimba na upatikaji wa chakula,Uendeleshwani wa miradi
iliyokwama kwenye ngazi ya shule “Alisema .
Aidha pia
alisema wakati wakianza kutekeleza mradi huo kwenye kata ya Segera wilayani
humo kulikuwa na changamoto kubwa sana na utoro kwa wanafunzi ambao walikuwa
wakiacha kwenda shule na kwenda kupakia machungwa kwenye malori lakini kwa sasa
jambo hilo limepungua kwa kiasi kikubwa.
Post A Comment: